IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu/96

Aya za Kwanza Zilizoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW)

20:57 - July 31, 2023
Habari ID: 3477363
TEHRAN (IQNA) – Aya 5 za mwanzo za Surah Al-Alaq zinazosisitiza kusoma na kupata elimu ni aya za kwanza zilizoteremshwa na Malaika Jibril kwa Mtume Muhammad (SAW).

Al-Alaq ni sura ya 96 ya Qur'anI Tukufu ambayo ina aya 19 na iko katika 30 Juz. Ni Makki na ni Sura ya kwanza iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Katika aya ya pili ya Sura, Mwenyezi Mungu anasema kwamba alimuumba mwanadamu kutokana na Alaq (donge la damu) na kutokana na neno hili linakuja jina la sura.

Kwa mujibu wa wafasiri wa Qur'ani Tukufu , Mtume Muhammad (SAW) alipokuwa kwenye Pango la Jabal Al Nour la Hira, Malaika Jibril alimwendea na kumwambia: “Soma! Muhammad (SAW) alisema hakuwa msomaji. Jibril alimkandamiza Muhammad (SAW) hivyo kumsababishia kupoteza nguvu zake zote. Malaika Jibril alirudia ombi hilo tena na Muhammad (SAW) akawa na jibu lile lile.

Kisha Aya za Sura Al-Alaq zikateremshwa na Malaika Jibril kwa Mtume Muhammad (SAW): “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba (vitu vyote).”

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwendea na kumuomba mkewe amfunike nguo ili apumzike.

Dhamira ya jumla ya Surah Al-Alaq ni Tawhid , kuheshimu elimu na kalamu, na pia uhusiano kati ya mali ya kidunia na uasi wa mwanadamu.

Mwenyezi Mungu katika Sura anamwamrisha Mtume (SAW) asome kisha amzungumzie mwanadamu, pamoja na ukuu wake wote, kuwa ameumbwa kutokana na pande la damu lisilo na thamani. Kisha Sura inazungumza kuhusu mwanadamu kuelekea kwenye ukamilifu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kufahamu kalamu na elimu.

Sura pia inawazungumzia watu wanaoasi na inaashiria adhabu chungu kwa wale wanaowazuia watu wasifikie uongofu na kutenda mema.

Kisha inaamrisha kusujudu na kumkaribia Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Allamah Tabatabai katika Tafsiri ya Al-Mizan ya Quran Tukufu, amri ya Mwenyezi Mungu ya kusoma ni amri kwa Mtume (SAW) kusoma aya za Quran.

Habari zinazohusiana
captcha