IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 103

Sura Al-Asr: Njia Nne za Kukaa Mbali na Hali ya Hasara

22:38 - August 07, 2023
Habari ID: 3477396
TEHRAN (IQNA) – Qur’ani Tukufu, katika Sura Al-Asr, inasisitiza kwamba mwanadamu, katika maisha yake duniani, daima yuko katika hali ya hasara, lakini pia inatanguliza njia za kukaa mbali na hasara.

Sura Al-Asr: Njia Nne za Kukaa Mbali na Hali ya HasaraAl-Asr ni sura ya 103 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya tatu na iko katika 30 Juz.

Ni Makki na ni Sura ya 13 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la sura linatokana na neno Asr (wakati, wakati wa alasiri, zama) ambalo Mwenyezi Mungu anaapa kwalo katika aya ya kwanza.

Surah Al-Asr imesisitiza kuwa wanadamu wamo katika hasara, “isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana wao kwa wao kwa haki na wakausiana subira.

Neno Khusr (hasara), ambalo limesisitizwa katika Sura hii, limetumika mara 60 katika Qur'ani Tukufu. Mtu anaweza kupata hasara katika mambo ya kimwili na pia katika nyanja za kiroho, ambapo inamaanisha kupotea. Wakati wa kutaja Khusr, Qur'ani Tukufu mara nyingi inakusudia hasara ya kiroho.

Kwa mujibu wa Allamah Tabatabai, maisha ya hapa duniani ni mtaji alionao kila mtu na kwamba wanapaswa kuutumia mtaji huu kuandaa maisha ya akhera. Ikiwa imani na mienendo ya mwanadamu inategemea ukweli, aanajishughulisha na biashara yenye faida, lakini ikiwa atafuata uwongo na kujiepusha na matendo mema na kumwamini Mwenyezi Mungu, biashara yake itakuwa imejaa hasara na mwishowe atakosa Baraka ya akhera.

Mwanzoni mwa Sura, Mwenyezi Mungu anaapa kwa Asr. Wafasiri wa Qur'ani Tukufu wanasema Asr inahusu historia ya ubinadamu na pia maisha ya kila mtu. Kwa kuzingatia aya zifuatazo, inaweza kusemwa kuwa watu wako katika hasara kadri maisha yao yanavyopita (na wanashindwa kuitumia kujiandaa na akhera).

Wale wanaozingatia kanuni nne wanaweza kukaa mbali na maisha ya hasara. Hao ni “wale walio amini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri. (Aya ya 3)

Kwa kuzingatia aya hii, njia ya kutoka katika hasara ni kumwamini Mwenyezi Mungu, kutenda mema, kuwahimiza wengine kuilinda na kuifanyia kazi haki, na kuwataka wengine wawe na subira.

Habari zinazohusiana
captcha