IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /98

Qur'ani Inasemaje kuhusu ‘kiumbe mbaya kuliko wote’

11:31 - July 22, 2023
Habari ID: 3477319
TEHRAN (IQNA) – Qur’ani Tukufu inatoa tathmini ya makundi mbalimbali ya watu na kuwaainisha kulingana na mienendo na tabia zao.

Katika moja ya kategoria hizi, kuna kundi la watu wanaopinga ukweli kwa ukaidi na makazi yao ni kuzimu. Yamefafanuliwa katika Sura Al-Bayyinah ya Qur'ani Tukufu.

Al-Bayyinah ni sura ya 98 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 8 na iko katika Juzuu ya 30. Ni Madani na ni sura ya 100 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Al-Bayyinah, ambayo imekuja katika Aya ya kwanza na ya nne na kuipa Sura jina lake, ina maana ya uthibitisho ulio wazi.

Allamah Tabatabaei anasema kwamba lengo kuu la Sura ni kusisitiza utume wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Anasema kuwa matendo safi ya ibada na imani juu ya ulazima wa kutii amri za Mwenyezi Mungu, ambazo Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amewaalika kila mtu kuzifanya, ndizo zinazounda dini inayolinda maslahi ya jamii ya wanadamu.

Surah Al-Bayyinah inaelezea uadui, ukaidi na uhasama wa "watu wa kitabu" ambao wanakataa kukubali ukweli wa Uislamu na ujumbe wa Mtume (SAW).

Sura inawaita na wanafiki kuwa ni “wabaya kuliko viumbe vyote” ambao “watakaa milele motoni”. Pia inawapa habari njema waumini na watu wema kwamba wataingia peponi na kukaa humo milele. Surah Al-Bayyinah pia inahusu ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW) wa ulimwengu wote na ushahidi wake wa wazi. Sura hiyo pia imetaja hukumu mbili za Fiqhi (kisheria) kuhusu Sala na Zaka kuwa Wajib.

Watu wa Kitabu na makafiri walidai kabla ya ujio wa Uislamu kwamba hawataacha imani yao mpaka ije dalili wazi na Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini baada ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kutumwa na Mwenyezi Mungu kama mjumbe, walibadili msimamo wao na, isipokuwa wachache tu, walianza kumpinga na kukabiliana na Mtume (SAW) ingawa Uislamu unawaamrisha watu kumwabudu Mwenyezi Mungu kikweli, kujiepusha na Shirki, kusimamisha sala na kutoa sadaka, ambazo ni kanuni zisizobadilika za imani zote za Mwenyezi Mungu.

Surah Al-Bayyinah pia inahusu hatima ya makafiri na waumini. Kundi la kwanza, ambalo linatambulishwa kuwa ni viumbe wabaya kuliko viumbe vyote, litakuwa motoni milele na kundi la pili, ambalo linatambulishwa kuwa bora zaidi ya viumbe vyote, litakuwa peponi milele kama malipo yao.  Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi Naye.

Habari zinazohusiana
captcha