IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /75

Kwa mujibu wa Surah Al-Qiyama , alama za vidole za mwanadamu ishara ya Mwenyezi Mungu

23:40 - May 07, 2023
Habari ID: 3476969
TEHRAN (IQNA) - Ukweli wa kushangaza ambao watu huchukulia kawaida ni kwamba alama za vidole za kila mtu ni tofauti na za wengine wote.

Huu ni ukweli wa kisayansi na Qur'ani Tukufu, katika Surah Al-Qiyama inairejelea kama ishara ya uwezo wa Mungu.

Jina la sura ya 75 ya Qur’ani Tukufu ni Al-Qiyama. Ina Aya 40 na imo katika Juzuu ya 29. Ni Makki na Sura ya 31 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Al-Qiyama maana yake ni Siku ya Kiyama. Ni siku ambayo watu wote huinuka kutoka makaburini mwao na kuelekea kwenye hatima yao ya milele, iwe peponi au motoni.

Katika aya ya kwanza ya Sura, Mwenyezi Mungu anaapa kwa Siku ya Kiyama na anawakumbusha watu siku hiyo. Jina la Sura linatokana na aya hii.

Sura inabainisha uhakika wa Siku ya Kiyama na inazungumzia jinsi inavyoonekana. Inasema watu wamegawanyika katika makundi mawili siku hiyo: Mmoja ambaye ana nyuso zenye kung'aa na mwingine mwenye nyuso zenye huzuni.

Sura inawakosoa wanaadamu kwa kuchagua dunia na kusahau akhera, ikibainisha kuwa watajuta siku ya kiama.

Inasema “Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.” (Aya ya 14) kama wanatoa visingizio au kukana makosa yao.

Sura hiyo pia inawaambia waliokanusha ambao wanatilia shaka uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kuwafufua na hali Yeye amekwisha wahuisha kutoka katika utupu.

“Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? .Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!" (Aya ya 3 na 4)

Aya hizi ziliteremshwa wakati mmoja wa majirani wa Mtukufu Mtume (SAW) alipomuuliza vipi Mungu ataikusanya mifupa ya wafu. Mungu anasema hapa kwamba si mifupa tu bali hata alama za vidole zitarejeshwa.

Wakati huo hakukuwa na ujuzi kuhusu watu kuwa na alama za vidole tofauti. Imegunduliwa hivi karibuni na wanasayansi kuthibitisha kwamba kila mtu ana alama ya vidole ya kipekee.

captcha