IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 101

Siku ambapo milima itakuwa kama sufi zilizochambuliwa

22:27 - July 29, 2023
Habari ID: 3477356
TEHRAN (IQNA) – Moja ya alama za Siku ya Kiyama ni hali ya kuchanganyikiwa katika ardhi ambapo milima itakuwa laini kama sufi.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Sufi ni jina kwa nyuzi laini kama pamba zinazotoka kwenye matunda ya msufi.

Kinachotokea siku hiyo ni kikubwa kuliko tetemeko lolote la ardhi na imeelezwa katika Surah Al-Qari’ah.

Al-Qari’ah ni sura ya 101 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 11 na iko katika sura ya 30. Ni Makki na ni Sura ya 30 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Baadhi ya wafasiri wanasema Siku ya Kiyama inaitwa Al-Qari’ah (kuponda) kwa sababu inaziponda nyoyo kwa khofu na kuwaponda maadui wa Mwenyezi Mungu kwa adhabu. Inaweza pia kuzingatiwa kuwa siku hiyo, ulimwengu utapondwa.

Surah hii inaashiria masuala makuu matatu: Kwamba Ufufuo ni tukio kubwa na la kuponda; kwamba watu watatawanyika na kuchanganyikiwa siku hiyo; na kwamba matendo ya watu yatapimwa na kupimwa kwa mizani maalum.

Tangu mwanzo hadi mwisho, Surah hii inazungumzia yale yatakayotokea Siku ya Kiyama na yale ambayo watu watapitia na kukabili siku hiyo.

Wale ambao wema wao ni zaidi ya dhambi zao wataishi maisha ya raha milele na wale waliokuwa na matendo maovu na dhambi nyingi kuliko wema wataingia motoni.

Sura inaashiria matukio mawili makubwa na ya kutisha Siku ya Kiyama.

" Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;" (Aya ya 4) Kwa kuzingatia Aya hii, watu hutawanyika na kukimbiana wao kwa wao siku hiyo.

Pia katika Siku ya Ufufuo, “ Na milima itakuwa kama sufi (pamba) zilizo chambuliwa!.” (Aya ya 5)

Nukta nyingine iliyotajwa katika Sura hii ni kwamba ili kupata wokovu na pepo, mtu anapaswa kutenda na kuishi katika ulimwengu huu kwa namna ambayo ili kustahiki kuingia peponi.  "Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza." (Aya za 6-7)

Matumizi ya neno mizani katika umbo la wingi katika Aya ya 6 inaweza kuwa kwa sababu siku hiyo, amali za mtu zitapimwa kwa njia mbalimbali na kwamba kutakuwa na mizani maalum ya kupima kila kitendo.

Habari zinazohusiana
captcha