IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu/ 102

Surah At-Takathur inayonyesha mbio Isiyo na thamani ya Wanadamu katika mambo ya kidunia

10:34 - August 05, 2023
Habari ID: 3477383
TEHRAN (IQNA) – Wanadamu wanasukumwa na tamaa ya kuwa na vitu vingi zaidi na zaidi vinavyowafanya wajisikie bora kuliko wengine. Hii inawaweka katika msako usio na mwisho na usio na maana wa vitu ambavyo havina thamani halisi, na kuwaondoa kutoka lengo lao halisi katika maisha ya dunia.

Sura ya 102 ya Qur'ani Tukufu inaitwa "Takathur". Sura hii ina Aya 8 na iko katika Juzuu ya 30 ya Qur'ani Tukufu. "Takathur" ni moja ya sura zilizoteremshwa huko Makka kwa Mtume Muhammad (SAW).

Neno "Takathur" maana yake ni kushindana na kujivunia mali na madaraka. Neno hili limetumika katika sura ya kwanza, na hapo ndipo sura hii inapopata jina lake.

Neno "Takathur" limetajwa mara mbili ndani ya Qur'ani Tukufu; Katika aya ya kwanza ya Surah Takathur na aya ya 20 ya Surah al-Hadid. Wafasiri wengine wanasema neno hilo hubeba dhana ya kuendelea. Kwa hivyo, kinachokosolewa katika Surah Takathur ni ushindani unaoendelea na mapambano ya kukusanya mali na kupata hadhi ya kijamii.

Ujumbe wa sura hii ni kulaani watu wanaoshindana wao kwa wao kwa mambo yasiyo na thamani. Kisha inawaonya kuhusu Siku ya Kiyama na moto wa Jahannamu, na kuwakumbusha kwamba wataulizwa kuhusu neema alizowapa Mwenyezi Mungu.

Surah Takathur inakemea watu kwa kushindana katika kukusanya mali, watoto, marafiki, na washirika. Tabia hii inawaweka mbali na Mwenyezi Mungu na furaha ya kweli. Sura hii pia inawaambia kwamba hivi karibuni wataona matokeo ya shughuli zao za ubatili, na wataulizwa kuhusu baraka walizozipata.

Surah hii pia inahusu makabila yaliyokuwa yakihesabu mali zao na idadi ya watu ili kuonyesha ubora wao kwa wengine, na walikuwa wakijivunia suala hili.

Kulingana na sura hii, mashindano haya yasiyo na maana huwafanya watu wamsahau Mwenyezi Mungu, Siku ya Hukumu, na lengo kuu la wanadamu.

Baadhi ya wafasiri wamezingatia aya hizi mbili zilizo na neno “Takathur” kuwa ni marudio yanayosisitiza jambo lile lile; wote wawili wanafahamisha kuhusu adhabu zinazowangoja watu wenye kiburi.

Wakati baadhi ya wafasiri wameichukulia Aya ya kwanza kuwa ni marejeo ya adhabu ya kaburini, na ya pili kuwa ni marejeo ya adhabu ya Akhera. "Kumekushughulisheni kutafuta wingi, Mpaka mje makaburini!."

Kutokana na sura hii, tunaweza kuhitimisha kwamba sababu kuu ya kiburi na kujionyesha ni kutojua malipo na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na kukosa imani katika Siku ya Hukumu.

Pia, watu wanapokabiliana na kushindwa na udhaifu, wanaelekea kwenye majivuno na kiburi cha uwongo.

Habari zinazohusiana
captcha