IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /108

Baraka Kuu ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume Mtukufu Imetajwa katika Sura Al-Kawthar

16:13 - August 22, 2023
Habari ID: 3477478
TEHRAN (IQNA) – Mwenyezi Mungu katika Sura Al-Kawthar ya Qur’ani Tukufu anazungumza kuhusu neema kubwa aliyopewa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Al-Kawthar ni sura ya 108 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya tatu na iko katika Juzuu ya 30. Ni Makki na ni Sura ya 15 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Aya ya kwanza inazungumza juu ya Kawthar, baraka aliyopewa Mtume Muhammad (SAW), na hivyo jina la Sura.

Kawthar maana yake ni baraka tele. Pia ni jina la mto ulio peponi. Sura inarejelea neema ambayo Mwenyezi Mungu amempa Mtume (SAW).

Kuna maoni tofauti kuhusu baraka hii ni nini, na wengine wanasema inahusu Uislamu, Qur'ani Tukufu, utume, idadi kubwa ya wafuasi, nk.

Wafasiri wengi wa Qur'ani Tukufu wanaamini kwamba inarejelea kwa binti wa Mtume (SAW), Bibi Fatima Zahra (SA) kwa sababu Sura inazungumza kuhusu wale waliomwita Mtukufu Mtume (SAW) Abtar (bila ya vizazi) kwa sababu hakuwa na watoto wa kiume. Mwenyezi Mungu aliteremsha Sura hii kwa kuwajibu.

Aya zote za sura hii zinazungumza na Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ili kumpa moyo katika kukabiliana na matatizo na kejeli istihzai za makafiri.

Sura inaanza kwa kusema: " Hakika tumekupa kheri nyingi' ikiwa ni kumbashiria Mtume Muhammad (SAW) kuhusu neema aliyopewa, ikimtaka amsifu na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hiyo kubwa na muhimu. Katika aya ya pili, kumwomba Mwenyezi Mungu na kutoa dhabihu kunatajwa kuwa njia ya kumshukuru Mwenyezi Mungu. “Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.”

Jambo moja katika aya hii ni msisitizo juu ya ukweli kwamba kusema sala, kutoa sadaka ya kuchinja, na matendo mengine ya ibada ni kwa ajili ya Mungu, ambaye ameumba baraka zote.

Hayo yalisemwa wakati ambapo baadhi ya watu waliabudu sanamu na miungu ya uwongo na kutoa dhabihu kwa ajili yao. Aya ya 3 ya Surah Al-Kawthar isemayo: " Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu", inahusu waliomtukana na kumkejeli Mtume (SAW) na kusema yeye ni Abtar. Aya hiyo inasema kwamba mkosaji mwenyewe hivi karibuni atakuwa hana mtoto na hana kizazi.

Habari zinazohusiana
captcha