IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /68

Sura Al-Qalam: Mwenyezi Mungu Anaapa kwa Kalamu Na Anayoyaandika

22:07 - March 15, 2023
Habari ID: 3476708
TEHRAN (IQNA) – Kalamu na inachokiandika ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu. Katika Qur'ani Tukufu, Mwenyezi Mungu ameapa kwa baraka hizi ili kuashiria umuhimu wake.

Al-Qalam ni jina la sura ya 68 ya Qur'ani Tukufu, ambayo ina aya 52 na iko katika Juzuu ya 29. Ni Makki na sura ya pili iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno al-Qalam (kalamu) katika Aya ya kwanza ambayo Mwenyezi Mungu anaapa kwa kusema: “…Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo. ”

Katika tafsiri yake ya Al-Mizan ya Qur'ani Tukufu, Allamah Tabatabai anasema hapa hairejelewi kalamu maalum au jambo lolote mahususi linaloandikwa bali makusudio ni kalamu yoyote na maandishi yoyote. Kwa hiyo kalamu na inachokiandika ni miongoni mwa neema kuu za Mwenyezi Mungu anazoapa nazo kama anavyoapa kwa neema nyinginezo ndani ya Qur'ani Tukufu kama vile jua, mwezi, mchana na usiku, na hata mtini na mizeituni.

Makusudio ya Sura hii ni kueleza sifa za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kutilia mkazo sifa zake tukufu za kimaadili, pamoja na tabia zisizofaa za makafiri na maadui wa Mtume (SAW).

Vile vile imesimulia kisa cha wamiliki wa bustani, inawaonya Musrikeen (washirikina) kuwakumbusha Siku ya Kiyama na adhabu zinazowangoja makafiri, inamuamrisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa imara dhidi ya makafiri na makatazo yanayowafuata.

Sura inamhakikishia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya wao kumtuhumu bila msingi. Sura imeharamisha kuwafuata Mushrikeen au kuwa mwenza wao.

Sura pia inazungumzia kuwapa muda makafiri na madhalimu, jambo ambalo hatimaye ni kwa hasara yao.

Kisha kuna kisa cha watu wa Peponi na yaliyo wapata baada ya kumsahau Mwenyezi Mungu na kutumbukia katika madhambi na ufisadi.

Ni simulzi ya watu kadhaa matajiri ambao walikuwa na bustani nzuri huko Yemen. Bustani hiyo kwanza ilikuwa ya mzee ambaye alitumia sehemu za mazao yake na kuwapa maskini. Baada ya kifo chake, wanawe waliamua kuweka mazao yote na kuwanyima wahitaji. Kutokana na ubahili wao, radi ilipiga bustani na moto ukatokea na kuharibu kila kitu.

Ndugu mmoja aliwaalika wengine wamkumbuke Mungu na wakajutia tabia zao na kutubu.

captcha