IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Jumuiya ya Qur'ani ya Iran yalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Uswidi

16:37 - July 04, 2023
Habari ID: 3477235
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Qur'ani Tukufu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali kitendo cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi, na kubainisha kuwa kukitukana kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu ni kuwatukana Mitume wa Mwenyezi Mungu na maandiko matakatifu.

Makumi ya makari na wahifadhi na vilevile maafisa wa taasisi za Qur'ani Tukufu walijumuika jana Jumatatu mbele ya ubalozi wa Uswidi mjini Tehran ili kuwasilisha malamiko yao makali baada ya mtu mmoja kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu siku ya Jumatano huko Stockholm.

“Kuitukana Qur'ani Tukufu ni tusi kwa wema wote, uzuri, elimu, nuru, na wema wa kibinadamu, na mitume na vitabu vitakatifu. Bila mafundisho ya Qur'ani Tukufu na utamaduni unaotokana nayo, jamii ya mwanadamu ingekuwa imetumbukia katika ujinga, dhulma na ukandamizaji tangu zamani," ilisema taarifa ya jumuiya hiyo.

"Si kweli kuwa chanzo cha matukio haya kinatokana na serikali fisadi au watu wabaya. Nyuma ya maovu haya, tunaweza kuona mikono ya watu binafsi wenye kiburi, watawala, ikiwa ni pamoja na Wazayuni, ambao wamekuwa wakijaribu kukandamiza jumuiya ya kimataifa kwa miongo kadhaa. Leo, wanaona msingi wao ukiporomoka mbele ya ushawishi unaozidi kupanuka wa Qur'ani Tukufu na mafundisho yake ya uhai,” walisema.

"Wadhalimu wa dunia wanafahamu kwamba mafundisho ya Qur'ani Tukufu yatadhoofisha harakati zao za kikatili, na kuwaongoza kujibu kwa majibu ya kitoto na maovu," iliongeza jumuiya hiyo.

“Ukweli kwamba adui analenga Qur’ani Tukufu inadhihirisha nia yao mbaya ya kutokomeza ustaarabu wa Kiislamu na kubomoa misingi ya Uislamu. Ni muhimu kutambua mpango wao tata na mpana na kukabiliana nao ana kwa ana,” ilisema taarifa hiyo.

Kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, ambayo kibali chake kilitolewa na mamlaka ya Uswidi, kumeibua maandamano na lawama kote ulimwenguni. Waandamanaji wameitaka Stockholm kuzuia kutoa vitendo hivyo vya kufuru.

3484198

 

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha