IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ajibu barua ya Ayatullah Sistani kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

17:26 - July 28, 2023
Habari ID: 3477349
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameijibu barua aliyoandikiwa na Kiongozi wa juu wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Uswidi na Denmark.
Katika barua yake hiyo ya majibu kwa barua aliyoandikiwa na Ayatullah Seyed Ali Sistani, Marjaa-Taqlidi wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq kuhusiana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Uswidi na Denmark, Guterres amelaani kitendo hicho kiovu na kutangaza mshikamano wake na Jamii ya Kiislamu katika suala hilo.
 
Kufuatia vitendo viovu vya kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu vilivyofanywa katika nchi za Uswidi na Denmark, Ayatullah Sistani alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo mbali na kulaani vitendo hivyo vya kishenzi vilivyofanywa katika nchi hizo mbili za Ulaya alisisitiza kuwa, kuheshimu uhuru wa kujieleza hakuwezi kwa namna yoyote kuwa sababu ya kutoa kibali cha kufanywa kitendo kama hicho cha kuaibisha.

Ayatullah Seyed Ali Sistani aliutaka pia Umoja wa Mataifa uchukue hatua madhubuti na athirifu ili kuzuia kurudiwa kwa vitendo hivyo viovu.

Siku ya Alhamisi, Julai 20, kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha wiki chache tu, raia wa Iraq na Uswidi  Salwan Momika aliivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa msaada wa polisi ya Polisi ya Uswidi; kitendo cha kitenzi cha kishenzi ambacho kilikabiliwa na mjibizo mkubwa wa nchi za Kiislamu.
 
Hivi karibuni pia, wanachama wa kundi lenye misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu la mrengo wa kulia wenye mielekeo ya kufurutu mpaka nchini Denmark liitwalo Patriots of Denmark waliuchoma moto Msahafu mbele ya ubalozi wa Iraq na wakafanya hivyo tena mbele ya balozi za Misri na Uturuki mjini Copenhagen.

4158523

Habari zinazohusiana
captcha