IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Uswidi yatafakari marufuku ya kuchoma moto Qur’ani Tukufu baada ya kilio cha ulimwengu

23:17 - July 07, 2023
Habari ID: 3477251
STOCKHOLM (IQNA) - Waziri wa Sheria wa Uswidi, Gunnar Strommer alisema serikali inafikiria kupiga marufuku kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu au vitabu vingine vya kidini baada ya kitendo cha kuchoma moto Qur’ani Tukufu hivi karibuni nchini humo kusababisha hasira katika Ulimwengu wa Waislamu.

Mtu mmoja alichoma moto kurasa za Qur’ani Tukufu nje ya msikiti huko Stockholm siku ya kwanza ya Eid Ul Adha, na kusababisha hasira katika ulimwengu wa Waislamu.

Maafisa wa Usalama Uswidi wanasema kwamba hatua kama hiyo inahatarisa usalama wa nchi.

Mahakama za Uswidi zimeunga mkono vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu kwa madai kwamba vitendo kama hivyo vinalindwa chini ya sharia ya uhuru wa kujieleza.

Hatahivyo akizungumza na gazet la  Aftonbladet, Strommer alisema Alhamisi kwamba serikali ilikuwa inachambua hali hiyo na kuzingatia ikiwa sheria inahitaji kurekebishwa.

Tukio hilo pia limeharibu jaribio la Uswidi ya kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO, kwani Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, nchi yake, ambayo ni mwanachama wa NATO, haiwezi kuridhia maombi ya Uswidi kutokana na vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur’ani nchini humo.

Wakati huo huo, uchunguzi mpya uliofanywa kwa niaba ya runinga wa kitaifa wa Uswidi umegundua kuwa raia wengi wa Uswidi sasa wanaunga mkono marufuku ya kuchomwa kwa maandishi ya kidini, kama vile Qur’ani Tukufu au Bibilia.

Uchunguzi huo, uliofanywa na Kantar Public, ulibaini kwamba asilimia 54 ya washiriki wanaamini kwamba kuchoma maandiko matakatifu hadharani kunapaswa kupigwa marufuku, wakati asilimia 34 wanaamini inapaswa kuruhusiwa, na asilimia 13 hawakuwa na maaoni. Hii inaashiria ongezeko la asilimia 11 kwa wale wanaopendelea kupiga marufuku vitendo kama hivyo tangu Februari mwaka huu, wakati uchunguzi kama huo ulifanywa.

3484244

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha