IQNA

Kutetea Qur'ani Tukufu

Ijumaa za Qur'ani zapangwa Misri kujibu vitendo vya kufuru nchini Uswidi

15:33 - July 19, 2023
Habari ID: 3477306
CAIRO (IQNA) - Wizara ya Awqaf ya Misri itakuwa na programu maalum ziitwazo 'Ijumaa ya Qur'ani' kila wiki ili kukabiliana na vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi.

Wizara hiyo imesema programu hizo zinazojumuisha duru za Qur'ani zitaandaliwa katika misikiti kote katika nchi hiyo.

Ijumaa hizo zimepengwa kufuatia ombi la wananchi waumini kama jibu la kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu nchini Uswidi, iliongeza, El-Balad News.

Mpango huo utaanza Ijumaa, Julai 23, baada ya sala ya Ijumaa, katika misikiti mikubwa ya miji, ilibainisha taarifa hiyo.

Wizara hiyo ilisema kuwa mapokezi mazuri ya duru za usomaji wa Qur'ani Tukufu yaliyofanyika tarehe 14 Julai yaliifanya ipange kuandaa matukio zaidi ya aina hiyo.

Ijumaa iliyopita, misikiti nchini Misri iliandaa duru 2,451 za Qur'ani katika miji tofauti ya Misri, iliongeza.

Mwishoni mwa Juni, mtu mwenye msimamo mkali alichoma Qur'ani Tukuf nje ya Msikiti Mkuu wa Stockholm kwa ulinzi wa polisi.

Alipanga kitendo chake cha kuudhi kuendana na Eid al Adha, sikukuu kuu ya Waislamu ambayo husherehekewa na wafuasi wa Uislamu duniani kote.

Polisi walikuwa wamempa kibali kwa msingi wa haki za uhuru wa kusema, lakini baadaye wakatangaza kwamba walikuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu “kuchafuka.”

Kitendo hicho cha kutoheshimu kilichochea hasira na kulaaniwa na nchi nyingi za Kiislamu, kama vile Iran, Uturuki, Saudi Arabia, Jordan, Palestina, Morocco, Iraq, Pakistan, Senegal, Morocco, na Mauritania.

3484395

captcha