IQNA

Hafidh wa Qur'ani

Kijana wa Nigeria azawadiwa tiketi ya Hija kwa ustadi wake wa kuhifadhi Qur'ani

11:09 - April 27, 2024
Habari ID: 3478741
IQNA - Bodi ya Ustawi wa Mahujaji wa Jimbo la Kano nchini Nigeria imemtunuku zawadi ya tiketi ya Hija kina Ja’afar Yusuf mwenye umri wa miaka 16 kwa sababu ya ujuzi na ustadi wake wa kuhifadhi Qur'ani.

Bodi hiyo ilisema zawadi hiyo imetokana na uwezo wake wa ajabu wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na ufahamu wake wa kina wa yaliyomo.

Akizungumza kwa niaba ya Gavana Abba Yusuf, mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo, Alhaji Laminu Danbappa, aliangazia kipaji cha kipekee cha Ja'afar, akibainisha kuwa kujitolea kwake kwa imani na ufahamu wake usio na kifani wa kila neno na muktadha wake ndani ya Qur'ani umewavutia wengi.

Katika taarifa iliyotolewa na afisa habari wa bodi hiyo, Sulaiman Dederi, gavana Yusuf alimpongeza kijana huyo kwa kujitolea, ustahimilivu, na umilisi wa Quran.

Alisisitiza umuhimu wa kukuza na kusaidia vipaji vya vijana kama Ja'afar. "Kutunukiwa Yusuf Ja'afar zawadi ya tiketi ya Hija ni ishara ya kutambua na kuthamini mafanikio yake ya kipekee katika usomaji wa Qur'an na dhamira yake isiyoyumba katika elimu ya kiroho," taarifa hiyo ilibainisha.

3488091

captcha