IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Kutukana matukufu ya kidini ni tishio la msingi wa kuishi pamoja kwa amani

14:48 - July 09, 2023
Habari ID: 3477257
ABUJA (IQNA) - Mwanaharakati wa Kiislamu wa Nigeria amelaani kitendo cha hivi karibuni cha kuvunjiwa heshima Qur'ani nchini Uswidi (Sweden) na kusisitiza kwamba vitendo hivyo vya kufuru vinatishia msingi wa kuishi pamoja kwa amani katika jamii.

Abdul Naghi, afisa wa Wakfu wa Al-Taghrib katika Jimbo la Bauchi la Nigeria, katika ujumbe wa video uliotumwa kwa Shirika la Habari la IQNA alishutumu vikali "kitendo cha kichaa na cha uchochezi cha kuchoma Qur'ani Tukufu" nchini Uswidi

"Sisi vile vile tunalaani mahakama (ya Uswidi) kwa ruhusa yake isiyo na msingi na isiyojali uvunjifu wa haki za mamilioni ya Waislamu, kugusa hisia zao kwa jina la uhuru wa kujieleza," aliongeza.

Amehoji hivi, je, ingewezekana “kwa kisingizio chochote kwa sababu yoyote ile hakimu huyu au mahakama hii hii (nchini Uswidi) kutoa ruhusa kwa mwendawazimu yeyote kuchoma Katiba ya Uswidi au bendera yake ya taifa… kwa jina la haki au kwa jina la uhuru wa aina yoyote?”

Mwanaharakati wa Kiislamu wa Nigeria alielezea kuchomwa kwa Kitabu Kitakatifu cha Uislamu kama hatua isiyo ya kistaarabu ambayo inaweza kudhoofisha kuishi pamoja kwa amani miongoni mwa jamii za Uswidi au katika nchi zingine.

"Jueni kwamba vitendo hivi vya kipumbavu havitashusha thamani ya Kitabu hiki Kitakatifu kwa vyovyote vile," alisisitiza.

Mnamo tarehe 29 Juni, mtu mmoja Mswidi mwenye umri wa miaka 37 anayeitwa Salwan Momika alichoma kurasa za Qur'ani Tukufu nje ya msikiti mmoja huko Stockholm katika siku ya kwanza ya Eid al-Adha.

Polisi wa Uswidi walikuwa wametoa kibali hapo awali kwa kitendo hicho cha kufuru.

Kitendo hicho kilizua hasira kubwa miongoni mwa Waislamu duniani kote na kulaaniwa kutoka nchi 

 

4153371

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha