IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Wapakistan waandamana kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko Uswidi

22:37 - July 07, 2023
Habari ID: 3477250
ISLAMABAD (IQNA) - Waislamu kote Pakistan walijitokeza mitaani Ijumaa kuandamana kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu nchini Uswdi.

Maandamano ya kitaifa yamekuja baada ya  wito wa Waziri Mkuu Shehbaz Sharif ambaye ametaka Wapakistan waadhimishe Siku ya Utakatifu ya Qur’ani baada ya tukio la Stockholm, Uswidi.

Mikutano mikubwa ilifanyika katika miji mikubwa ya nchi ikiwemo Karachi na Lahore baada ya sala za Ijumaa.

Katika mji mkuu wa Islamabad, mawakili walioshikilia nakala za Qur’ani Tukkufu waliandamana mbele ya Mahakama Kuu huku waumini wengine wakikusanyika nje ya misikiti wakitaka kutengana kwa uhusiano wa kidiplomasia na Uswidi.

Kundi la Wakristo ambao wako katika jamii ya  wachache kaskazini magharibi mwa Pakistan pia walifanya mkutano wa kukemea kuchomwa kwa Qur’ani Tukufu nchini Sweden.

Hasira imeenea katika nchi za Waislamu tangu Jumatano iliyopita wakati mtu aliyetambuliwa katika vyombo vya habari vya Uswidi kama Mkristo kutoka Iraq alichoma nakala ya Qur’ani Tukufu nje ya msikiti huko Stockholm wakati wa likizo ya kidini ya Eid al-Adha.

Katika hotuba ya televisheni kwa wabunge katika Bunge Alhamisi, Sharif alihoji ni kwanini polisi huko Uswidi waliruhusu kuchomwa kwa Qur’ani Tukufu.

Aidha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa pia linatarajiwa kufanya mkutano wa haraka mnamo Julai 11 juu ya "kuongezeka kwa kutisha kwa vitendo vya umma vya chuki za kidini".

3484242

Habari zinazohusiana
Kishikizo: uswidi qurani tukufu
captcha