Katika ujumbe wake wa Twitter, alisema tukio hilo la uchungu limeumiza sana hisia za mabilioni ya Waislamu. Rais wa Pakistani alisema kila taifa lazima lichukue hatua za kuzuia vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu.
Aliitaka jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kwa ajili ya kukuza maelewano kati ya dini na mazungumzo ili kujenga kuvumiliana kwa imani na maadili ya kidini ya kila mmoja.
Alvi alisisitiza kuwa ubinadamu lazima uondokane na vitendo vya chuki zisizo na maana kuelekea kuunganisha ulimwengu kwa amani.
Mataifa mengi ya Waislamu kama Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Iraq, Saudi Arabia, Kuwait, Pakistan, Jordan na Uturuki yametoa taarifa za kulaani kitendo hicho cha kuvunjiwa heshima Qurani Tukufu nchini Uswidi siku ya Jumatano wakati wa kuanza siku kuu ya Idul Adha.