IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Nchi za Kiarabu zapongeza marufuku kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark

16:57 - December 19, 2023
Habari ID: 3478056
IQNA - Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imepongeza uamuzi wa hivi majuzi wa bunge la Denmark wa kuharamisha kunajisi maandishi ya kidini.

Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika taarifa yake imeeleza hatua hiyo kuwa ni hatua ya kuwajibika ambayo itajenga mazingira ya kuaminiana, kuelewana, kuvumiliana na kukubalika na kuepuka misimamo mikali, ubaguzi wa rangi na chuki.

Taarifa hiyo ilisisitiza haja ya kukataliwa kwa kitendo chochote cha uchochezi dhidi ya matakatifu ya kidini na kuialika jumuiya ya kimataifa kuzingatia haki na usawa katika sheria.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hissein Brahim Taha naye alipongeza sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Denmark na kuitaja kuwa ni hatua nzuri katika huduma ya kuishi kwa amani, kuvumiliana na urafiki kati ya mataifa, jamii na wafuasi wa imani tofauti.

Bunge la Denmark limepitisha mswada wa sheria inayoharamisha vitendo vya kuvunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu katika maeneo ya umma.

Mapema Disemba, Bunge la Denmark lilipitisha mswada wa sheria inayoharamisha vitendo vya kuvunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu katika maeneo ya umma.

Vitendo kadhaa vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark miezi ya hivi karibuni vimezuia hasira miongoni mwa Waislamu katika majira ya kiangazi.

Muswada huo uliopitishwa  unakataza "vitendo visivyofaa kwa maandishi yenye umuhimu mkubwa wa kidini kwa jumuiya ya kidini inayotambulika."

Muswada huo ulilipitishwa kwa kura 94 za ndio na 77 za la katika bunge hilo lenye viti 179.

Kuchoma, kurarua, au kunajisi maandishi ya kidini hadharani kunaweza kusababisha watu kutozwa faini au kufungwa hadi miaka miwili gerezani. Kuharibu maandishi matakatifu kwenye video na kusambaza video mtandaoni pia kunaweza kupelekea mhusika au wahusika kufungwa jela.

Waziri wa Sheria Peter Hummelgaard ameszungumza baada ya kupitishwa muswada huo na kusema: "Lazima tulinde usalama wa Denmark na Wadenmark,"

Uswidi pia inazingatia jinsi ya kukabiliana na vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, lakini inachukua mtazamo tofauti na Denmark. Inachunguza uwezekano wa kuruhusu polisi kuzingatia usalama wa taifa wakati wa kuamua kuhusu maombi ya maandamano ya umma.

Vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya vimeibua hasira duniani na kupelekea Waislamu waanzishe kampeni kubwa ya kiuchumi ya kususia bidhaa za nchi husika hasa Uswidi, Denmark na Uholanzi jambo ambalo limepelekea mashirika ya kibiashara ya nchi hizo kupata hasara kubwa.

4188733

Kishikizo: qurani tukufu denmark
captcha