IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

OIC yalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark

16:16 - July 23, 2023
Habari ID: 3477325
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe wa kudumu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wenye makao yake katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisii umelaani vikali kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu katika mji mkuu wa Denmark Copenhagen.

Taarifa ya OIC imeeleza kuwa, kutetea mtawalia hatua hizi zilizo dhidi ya Uislamu na kutozuia vitendo hivyo kwa kisingizio eti cha uhuru wa kusema na kutoa maoni kwa hakika ni kuchochea kinga ya kutoadhibiwa wahusika wanaofanya vitendo viovu kama hivi.

Timu ya Uwakishi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) mjini Geneva imebainisha bayana kwamba, watu ambao licha ya kuweko maagizo ya wazi ya Haki za Binadamu lakini hawachukui hatua wanapoteza haraka heshima na itibari yao.

Tukio hili liinajiri huku ulimwengu wa Kiislamu ukiiendelea kupaza sautii za malalamiko kulaanii kitendo kingine cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu huko nchini Sweden.

Katika miaka ya hivi karibuni Denmark na Uswidi zimegeuka kuwa chaka la maadui wa Uislamu ambao wamekuwa wakiendesha kampeni za chuki dhidi ya Uislamu.

Katika upande mwingine, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark.

Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq nayo imelaani vikali kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark na kuitaka jamii ya kimataifa kusimama kidete kukabiliana na utovu wa adabu huo.

Baada ya raia mmoja wa Sweden kuivunjia heshima tena Qur'ani Tukufu mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Stockholm Alkhamisi iliyopita, genge jingine lenye misimamo mikali ya kulia limemuunga mkono mtenda jinai huyo kwa kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Copenhagen, Denmark.

3484446

Habari zinazohusiana
Kishikizo: denmark qurani tukufu
captcha