IQNA

Uislamu Ulaya

Bunge Denmark laidhinisha marufuku vitendo ya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu

11:05 - December 08, 2023
Habari ID: 3478003
Bunge la Denmark limepitisha mswada wa sheria inayoharamisha vitendo vya kuvunjia heshima nakala za Qur'ani Tukufu katika maeneo ya umma.

Vitendo kadhaa vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Denmark miezi ya hivi karibuni vimezuia hasira miongoni mwa Waislamu katika majira ya kiangazi.

Muswada huo uliopitishwa Alhamisi unakataza "vitendo visivyofaa kwa maandishi yenye umuhimu mkubwa wa kidini kwa jumuiya ya kidini inayotambulika."

Muswada huo ulilipitishwa kwa kura 94 za ndio na 77 za la katika bunge hilo lenye viti 179.

Kuchoma, kurarua, au kunajisi maandishi ya kidini hadharani kunaweza kusababisha watu kutozwa faini au kufungwa hadi miaka miwili gerezani. Kuharibu maandishi matakatifu kwenye video na kusambaza video mtandaoni pia kunaweza kupelekea mhusika au wahusika kufungwa jela.

Waziri wa Sheria Peter Hummelgaard ameszungumza baada ya kupitishwa muswada huo na kusema: "Lazima tulinde usalama wa Denmark na Wadenmark,"

Kabla ya sheria kuanza kutekelezwa, Malkia Margrethe anahitaji kutia sahihi mswada huo.

Mswada huo, uliotangazwa mwishoni mwa Agosti, ulifanyiwa marekebisho baada ya kukosolewa kwamba rasimu yake ya kwanza inabana uhuru wa kujieleza na itakuwa vigumu kutekelezwa.

Kulingana na takwimu za polisi wa Denmark, kulikuwa na vitendo  483 vya kuchoma moto vitabu au bendera kuanzia Julai 21 hadi Oktoba 24 nchini Denmark.

Uswidi pia inazingatia jinsi ya kukabiliana na vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, lakini inachukua mtazamo tofauti na Denmark. Inachunguza uwezekano wa kuruhusu polisi kuzingatia usalama wa taifa wakati wa kuamua kuhusu maombi ya maandamano ya umma.

Vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya vimeibua hasira duniani na kupelekea Waislamu waanzishe kampeni kubwa ya kiuchumi ya kususia bidhaa za nchi husika hasa Uswidi, Denmark na Uholanzi jambo ambalo limepelekea mashirika ya kibiashara ya nchi hizo kupata hasara kubwa.

3486328

Habari zinazohusiana
Kishikizo: denmark qurani tukufu
captcha