IQNA

Ombi la kukataa mswada unaopiga marufuku kudhalilisha Qur’ani Tukufu nchini Denmark

10:50 - October 05, 2023
Habari ID: 3477690
Vyama vya upinzani vya serikali ya Denmark viliwataka wawakilishi wao katika bunge la nchi hiyo kuhudhuria siku ya kupiga kura kupinga mswada uliopendekezwa unaokataza kudhalilisha matukufu ya dini.

Kulingana na IKNA, ikimnukuu Anatoly, vyama vitano vya upinzani vya Denmark vilitangaza Jumanne, mwezi Oktoba 11, kwamba vitakusanya idadi ya juu zaidi ya wawakilishi wao kupinga mswada wa serikali wa kuharamisha alama za matusi za kidini, kikiwemo kitabu kitukufu cha Waislamu.

 Mswada huu utapigiwa kura katika kikao cha bunge kilichoanza jana,siku ya Jumanne, baada ya likizo ya vuli ,Vyama vya Liberal Alliance, Denmark Democrats, Conservatives, Danish People's Party na Nai Bürgerlige vyama ambavyo vyote ni vyama vya mrengo wa kulia, viliwaomba wawakilishi wao kufika bungeni kadri wawezavyo ili kupinga sheria iliyopendekezwa na serikali kukabiliana na uchomaji wa Qur’ani Tukufu.

Stephen Larsen, msemaji wa sheria wa Muungano wa Kiliberali, alielezea kusikitishwa kwake na jinsi kura hiyo ilivyopigwa katika taarifa siku ya Jumanne, akisema anataka kuwasilisha picha wazi ya wafuasi na wapinzani wa sheria hiyo.

Mwezi Agosti 25, serikali ya mseto ya Chama cha Kidemokrasia cha Kijamii, Chama cha Liberal na wasimamizi wakuu walianzisha sheria ya kuharamisha alama za matusi za kidini, Sheria hiyo ilipitishwa baada ya kuchomwa moto Qur’ani Tukufu  mara kwa mara na mwanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Denmark Rasmus Paludan, mojawapo ambayo ilitokea karibu na msikiti na nje ya ubalozi wa Uturuki mjini Copenhagen mapema mwaka huu.

Kuchafuliwa kwa Qur'ani kulichochea hasira ya ulimwengu wa Kiislamu, na Uturuki ililaani vikali kuidhinishwa kwa kitendo hiki cha uchochezi na mamlaka na kukiona kuwa ni uhalifu wa chuki, Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark, iliyochapishwa baada ya kuwasilishwa muswada huu bungeni, ilielezwa;  Hatua hii inafanywa ili kuharamisha uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu.

Kutokana na kuchomwa moto kwa Qur'ani hivi karibuni, Denmark ilizidi kuonekana katika sehemu kubwa za dunia kama nchi inayowezesha vitendo vya matusi na udhalilishaji dhidi ya nchi na dini nyingine, ilisema taarifa hiyo.

Mswada haujumuishi usemi wa maneno au maandishi, ikijumuisha vikaragosi, lakini unalenga vitendo vinavyofanywa hadharani au kwa lengo la usambazaji na utangazaji mpana.

 Peter Humelgaard, Waziri wa Sheria wa Denmark, alisema; Vitendo hivi vya matusi na kudhalilisha vina athari mbaya kwa usalama wa Denmark, nje ya nchi na ndani ya Denmark,  alibainisha kuwa hii ina maana hasa kwamba kuchoma hadharani Biblia au Qur’ani  itakuwa kosa la jinai linaloadhibiwa.

Hata hivyo, tangazo la vyama vya upinzani linaweka wazi kuwa serikali haina uwezekano wa kupata idadi kubwa ya kura za kupitisha sheria hiyo bungeni, Sheria mpya itajumuishwa katika Sura ya 12 ya Kanuni ya Adhabu ya Denmark, ambayo inahusu usalama wa taifa, Adhabu ya kukiuka sheria inaweza kuanzia faini hadi miaka miwili jela.

 

4172921

Kishikizo: denmark qurani
captcha