IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu/11

Tafsiri ya kwanza ya Qur'ani Tukufu katika lugha ya Kialbania

16:13 - December 17, 2022
Habari ID: 3476263
TEHRAN (IQNA) - Fathi Mahdiyu ni msomi ambaye ametafsiri Kurani nzima kwa Kialbania huko Kosovo. Katika kitabu chake cha hivi punde zaidi ambacho kimetafsiriwa na kuchapishwa kwa Kiarabu hivi karibuni, anazungumzia mwenendo wa tafsiri ya Qur'ani katika nchi za Balkan.

Katika kitabu hiki, chenye anuani ya "Lugha ya Kiarabu katika Lugha ya Kialbania kuanzia 1921 hadi 2021", kilichotarjumiwa kwa Kiarabu na Ibrahim Fadlallah, Mahdiyu anazungumzia fasihi ya Kiarabu ambayo imetafsiriwa katika Kialbania katika kipindi cha miaka 100 iliyopita.

Mwandishi anaamini kwamba kuongezeka kwa idadi ya tarjumi kutoka Kiarabu hadi Kialbania katika miaka ya hivi karibuni ni ishara ya kuongezeka kwa hamu ya fasihi ya Kiarabu na juhudi za wasomi katika uwanja wa lugha ya Kiarabu haswa wahitimu wa idara ya masomo ya mashariki ambayo ilianzishwa katika Chuo Kikuu cha Pristina mwaka 1973.

Kitabu hicho kinasisitiza kuwa tarjuma ya fasihi ya Kiarabu katika lugha ya Kialbania ilianza mwaka 1921 baada ya kuchapishwa kwa tafsiri ya kwanza ya Qur'ani Tukufu mwaka 1921.

Kwa maneno mengine, Qur'ani Tukufu inajulikana kuwa yenye hadhi ya juu katika lugha ya Kiarabu na ni maandishi mazuri zaidi katika lugha hiyo kwa sababu ya muujiza na ufasaha wake na neno fasihi hapa linarejelea kila maandishi mazuri.

Inaonekana Fathi Mahdiyu katika kitabu hiki amefuata nyayo za mwalimu wake Hassan Kalshi (1922-1976) ambaye alifanya utafiti wa kiuchambuzi na kuandika makala yenye kichwa cha habari “The Qur'an, Greatest Work in Arabic Literature” ambayo ilichapishwa kwa lugha ya Kiserbia kama utangulizi wa kitabu "Nukuu kutoka kwa Qur'ani Tukufu" mnamo 1967.

Mahdiyu alitarjumi Qur'ani Tukufu kwa Kialbania katika Yugoslavia ya zamani ya kikomunisti wakati ambapo kupata nakala ya Qur'ani Tukufu ndani ya nyumba kungemfanya mwenye nyumba hiyo kufungwa jela. Hiyo  ilikuwa tarjumi yake ya kwanza kamili ya Qur'ani Tukufu katika Kialbania, mwaka 1985.

Kabla yake, watafsiri wengine, wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu, walikuwa wametoa tafsiri za Kitabu Kitakatifu cha Uislamu katika lugha nyinginezo za Balkan kama vile Kiserbia, Kibosnia na Kibulgaria.

Kufuatia kuondolewa kwa marufuku ya kutafsiri Qur'ani Tukufu, kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya kuitarjumi katika Kialbania jambo ambalo lilisababisha ushindani wa kutoa tafsiri bora zaidi.

3481699

captcha