IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Kiislamu Duniani/1

Sheikh Muhammad Sadiq Arjun, mtetezi wa Uislamu wa wastani

14:04 - October 09, 2022
Habari ID: 3475901
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Muhammad Sadiq Ibrahim Arjun alikuwa mwanazuoni wa Al-Azhar ambaye aliandika vitabu vingi vya taaluma za Kiislamu, kikiwemo kitabu kuhusu namna Uislamu unavyohimiza watu kuishi pamoja kwa amani.

Alizaliwa mwaka wa 1903 katika mji wa Jimbo la Aswan nchini Misri, Arjun alisoma katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar na kuhitimu mwaka wa 1929.

Kisha akaanza kufundisha katika vituo vinavyofungamana na Al-Azhar, ikiwa ni pamoja na moja huko Alexandria. Mnamo 1964, alikua mkuu wa Kitivo cha Lugha ya Kiarabu na Misingi ya Kidini.

Arjun pia alisafiri katika nchi kama Kuwait, Libya, Sudan, na Saudi Arabia kwa ajili ya utafiti na mafundisho, kuandika vitabu wakati wa kukaa kwake katika nchi hizo.

"Uthman ibn Affan", "Ali ibn Abi Talib, Mrithi Bora Mtukufu Mtume (SAW)", "Qur'an Adhimu na Mwongozo na Miujiza katika Matamshi ya Wafasiri", na "Njia ya Kutafsiri Qur'ani" ni majina ya baadhi ya vitabu vyake.

Kitabu chake kikuu alichotumia miaka kumi kukiandika na kuchapishwa katika juzuu nne ni “Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu; Mbinu na Malengo".

Inachukuliwa kuwa mojawapo ya kazi bora zaidi zilizoandikwa katika zama hizi kuhusu Sirah ya Mtukufu Mtume (SAW).

Katika kitabu hiki, Arjun ametoa uhakiki wa mitazamo ya wale ambao wamezua shaka juu ya Sirah.

Sheikh Arjun pia aliandika vitabu na makala kuhusu wahusika wa kidini kama Abu Hamid Al-Ghazali na maoni yake kuhusu Usufi na uhuru wa kujieleza.

Katika kitabu cha "An Encyclopedia on Islam's Coexistence", iliyochapishwa katika juzuu mbili, Arjun anafafanua juu ya namna Uislamu unavyohimiza Waislamu kuishi kwa maelewano na wasiokuwa Waislamu.

Baada ya miaka mingi ya juhudi za kukuza Uislamu na Qur'ani Tukufu, Sheikh Arjun alifariki mwaka 1981.

 

captcha