IQNA

Ahadi ya Kweli

Mufti wa Oman apongeza hatua ya Iran kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Israel

16:30 - April 16, 2024
Habari ID: 3478687
IQNA-Mufti Mkuu wa wa Oman amekaribisha na kupongeza mashambulizi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Ahmad bin Hamad al-Khalili ameandika ujumbe katika ukurasa wake binafsi katika mtandao wa kijamii wa X na kusema: Kilichochapishwa katika vyombo vya habari kuhusu ujasiri wa hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kujibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ubalozi mdogo wa Iran ni jambo la kufurahisha sana, na tunatumai litazaa matunda hivi karibuni.

Mufti wa Oman ameongeza kuwa: Tunapongeza kitendo hiki na vingine mfano wake na tunatumai kuwa vitalinda uwezo na uwepo wa Umma. Kwa sababu nguvu ya kujilinda ni muhimu sana kwa ajili ya kikabiliana na shari, vinginevyo, itaenea na kupanuka.

Sheikh Ahmad al Khalili amesema: Tunatumai kuwa yaliyotokea yatakuwa na uchungu na maumivu kwa Wazayuni na wale waliowasaidia, na tunasubiri kwa hamu kubwa jambo litakalovunja nguvu za Wazayuni, kuzima njama zao na kuwalinda Waislamu na shari yao.

Jumamosi  usiku na alfajiri ya Jumapili, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) lilianzisha "mashambulio makubwa" ya kulipiza kisasi kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ngome za kijeshi za utawala haramu wa Israel katika ardhi zinazokaliwa  kwa mabavu ili kulipiza kisasi shambulio la utawala wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus ambalo lilisababisha kuuawa shahidi maafisa saba wa IRGC mnamo Aprili 1.

IRGC ililitangaza kuzindua hujuma hiyo katika taarifa Jumamosi usiku, ambapo mashambulio hayo yalipewa jina  "Operesheni ya Ahadi ya Kweli".

Taarifa hiyo ilianza kwa aya ya 22 ya Surah As-Sajdah inayosomeka "…Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu…," IRGC na kuongeza kuwa: "Katika kujibu jinai nyingi za utawala wa Kizayuni, pamoja na shambulio la sehemu ya ubalozi wa Iran huko Damascus na kuuawa shahidi kwa baadhi ya makamanda na washauri wa kijeshi wa Iran nchini Syria, Kitengo cha Wanaanga cha IRGC kilirusha makumi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo kadhaa ndani ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel)."

Vile vile IRGC ilihitimisha taarifa yake kwa kunukuu Aya ya 126 ya Surah Al-Imran: “Na msaada (ushindi) hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima.                                                                                                         

 

4210670

 

captcha