IQNA

Qari Maarufu wa Misri

Sheikh Al-Bujairami wa Misri akisoma aya za Surah Al-Haqqa (+Video)

18:26 - January 17, 2024
Habari ID: 3478207
IQNA - Sheikh Mahmoud al-Bujairami alikuwa qari mashuhuri wa Misri ambaye alisafiri katika nchi nyingi za Kiislamu kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu.

Alizaliwa mwaka 1933 katika kijiji cha Bujairam katika Jimbo la Menofia nchini Misri. Katika utoto wa mapema, alianza kujifunza Qur'ani Tukufu na mafundisho ya kidini. Alifanikuwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu  na akajifunza sheria za Tajweed.

Baadaye alijiunga na taasisi ya Qur'ani Tukufu   ya Shibra ili kuimarisha ujuzi wake wa Qur'ani na kujifunza Qira'at (mitindo ya usomaji tofauti).

Kwa kuwa alikuwa na sauti nzuri na alikuwa stadi katika Lahn (matamshi sahihi ya maneno ya Qur'ani), al-Bujairami alianza kusoma Qur'ani katika programu tofauti na kufuata mtindo wa maqari maarufu wa wakati huo.

Alipendezwa sana na mtindo wa Lahn wa Sheikh Mustafa Ismail na, kwa hiyo, alianza njia yake ya Qur'ani Tukufu  kwa kuiga mtindo wa Sheikh Mustafa Ismail katika Lahn.

Alipopata umahiri wa kusoma, al-Bujairami alifanya mtihani katika Idhaa ya Qur'ani ya Misri mwaka 1986 na kujiunga na makari wengine mashuhuri wa redio hiyo baada ya kufaulu mtihani huo.

Alisoma Qur'ani Tukufu  katika studio na pia katika vipindi na vikao vya Qur'ani nje ya studio ambazo zilirushwa na Redio ya Qur'ani na kurushwa kwa wasikilizaji ndani na nje ya Misri.

Moja ya hafla za Qur'ani alizohudhuria mara kwa mara ni programu za usomaji wa asubuhi katika Msikiti wa Imam Hussein (AS) huko Cairo.

Mnamo 1966, alikua qari wa Msikiti wa Omar ibn Abdul Aziz huko Heliopolis, kitongoji cha Cairo na mnamo 1980 alichaguliwa kama qari wa Msikiti wa AIn al-Hayat.

Wakati huo alikuwa amepata umashuhuri na mara kwa mara alialikwa katika nchi mbalimbali za Kiislamu, zikiwemo Umoja wa Falme za Kiarabu kusoma Qur'ani Tukufu .

Vile vile aliitembelea Iran miaka michache kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kufanya kisomo kikubwa katika Msikiti wa Qoba wa Tehran na pia majumbani na vikao vya  Qur'ani lakini nyingi kati ya hizo hazikurekodiwa.

Baada ya miaka ya kutumikia Qur'ani Tukufu  na kutoa kazi nzuri katika uwanja huo, Sheikh Mahmoud al-Bujairami aliaga dunia mnamo 1992.

Hapa chini ni  kisomo chake aya 4 za kwanza za Surah Al-Haqqa:

Habari zinazohusiana
captcha