IQNA

Qarii Maarufu

Sheikh Mustafa Ismail; Qari mashuhuri kutoka Misri

17:18 - December 27, 2023
Habari ID: 3478102
IQNA - Disemba 26 ni kumbukumbu ya kifo cha mmoja wa wasomaji mashuhuri wa Qur'ani Tukufu nchini Misri.

Sheikh Mustafa Ismail alifariki miaka 45 iliyopita na ameacha historia kubwa katika usomaji wa Qur'ani Tukufu.

Alijulikana kama qari mwenye zoloto ya dhahabu, msomaji kutoka mbinguni na mfalme wa maqamat za Qur'ani Tukufu.

Mfalme Farouk wa Misri alimchagua kama qari wa jumba la kifalme. Misri ilipokuwa jamhuri, marais Gamal Abdel Nasser na Anwar Sadat pia walimtukuza Sheikh Mustafa Ismail.

Mustafa Ismail alizaliwa Juni 1905 katika kijiji kiitwacho Mit Gazal karibu na mji wa Tanta huko Gharbia nchini Misri.

Sheikh Mustafa Ismail; A Legendary Qari from Egypt

Wazazi wake walimwita Mustafa Muhammad Mursi Ismail. Baba yake, ambaye alikuwa mkulima, alimpeleka katika shule ya Qur'ani Tukufu inayoongozwa na Sheikh Abdul Rahman Abulainain kuhifadhi Quran.

Mustafa Ismail aliweza kujifunza Quran nzima kwa moyo akiwa na umri wa miaka 10.

Kisha akaanza kujifunza usomaji wa Kurani na kanuni za Tajweed na Sheikh Idris Fakhir.

Mara ya kwanza alisoma Qur'ani Tukufu mbele ya umati wa watu akiwa na umri wa miaka 14. Wale waliosikia kisomo chake kwenye Msikiti wa Atif huko Tanta walishangazwa na utendaji wake mzuri na wakamtia moyo aendelee na njia ya usomaji wa Qur'ani Tukufu. 

Alifanya hivyo kwa kwenda Cairo na kujifunza zaidi katika uwanja huo kutoka kwa Qari mashuhuri Sheikh Muhammad Rafa’at.

Punde si punde akawa Qari mashuhuri kote Misri na akasafiri katika nchi nyingine nyingi, zikiwemo Iraq, Indonesia, Saudi Arabia, Pakistan, Ujerumani, Palestina, Uingereza na Ufaransa kusoma Quran.

Sheikh Mustafa Ismail; A Legendary Qari from Egypt

Pia alipokea medali nyingi za heshima katika nchi yake na kwingineko. Sheikh Mustafa Ismail alifariki tarehe 26 Desemba 1978 na akazikwa nyumbani kwake.

Sheikh Mustafa Ismail; A Legendary Qari from Egypt

3486575

Kishikizo: mustafa ismail
captcha