IQNA

Qiraa ya mshindi wa kategoria ya kuhifadhi katika mashindano ya Qur'ani Tukufu nchini Malaysia

17:10 - August 30, 2023
Habari ID: 3477519
KUALA LUMPUR (IQNA)- Klipu ya mashindi wa kategoria ya kuhifadhi katika Mashindano ya 63 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia 2023 imesambazwa mitandaoni.

Kwa mujibu wa IQNA, Omar Toure, msomaji wa Guinea, alishika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ambapo hapa katika klipu hii anaonekana akisoma aya ya 80 na 81 za Surah Al-Imran isemayo, "Wala hatakuamrisheni kuwafanya Malaika na Manabii kuwa ni miungu. Je, atakuamrisheni ukafiri baada ya kuwa nyinyi Waislamu?  Na pale Mwenyezi Mungu alipo chukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikima, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: Je, mmekiri na mmekubali kushika agizo langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. Akasema: Basi shuhudieni, na Mimi ni pamoja nanyi katika kushuhudia."

Mashindano ya 63 ya kimataifa la Qur'ani la Malaysia yanayojulikana rasmi kama Mkutano wa Kimataifa wa Kusoma na Kuhifadhi Qur'ani ya Malaysia (MTHQA), ilifanyika hapa katika mji mkuu wa Malaysia yalifanyika wiki iliyopita Agosti 19 -24.

Jumla ya wawakilishi 76 kutoka nchi 52 walishindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika sehemu tofauti kwa wanaume na wanawake.

Wanaume 24 na wanawake 12 walishindana katika kitengo cha usomaji nyakati za jioni, na wanaume 27 na wanawake 13 katika kitengo cha kukariri kilichofanyika asubuhi.

Mashindano hayo yalirushwa moja kwa moja katika akaunti za mitandao ya kijamii za Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM).

Habari zinazohusiana
Kishikizo: malaysia
captcha