IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Qari wa Iran awavutia wengi katika mashindano ya 63 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia

KUALA LUMPUR (IQNA) – Alireza Bijani, mwakilishi wa Iran katika kategoria ya kisomo ya mashindano ya 63 ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia, amewavutyia wengi kwa qiraa yake Jumanne usiku.

Bijani alisoma baadhi baadhi ya aya za  Surah Al-A'raf, na kuuvutia umati wa watu katika ukumbi wa Kuala Lumpur World Trade Center kwa sauti yake tamu na usomaji usio na dosari.Qiraa yake ilikuwa ilirushwa hewani mubashara katika Televisheni ya Qur'ani ya Iran.

Jumla ya wawakilishi 76 kutoka nchi 52 wamepangwa kushindana katika kategoria mbili za usomaji na kuhifadhi Qur'ani. Kwa mujibu wa taarufa, wanaume 24 na wanawake 12 wanashindana katika kitengo cha usomaji ambacho kinafanyika jioni, na wanaume 27 na wanawake 13 katika kitengo cha kuhifadhi  kinafanyika  asubuhi.

Matukio yote ya mashindano hayo yanaonyeshwa moja kwa moja kutoka kwa akaunti za mitandao ya kijamii za Idara ya Maendeleo ya Kiislamu Malaysia (JAKIM). Mashindano hayo yatakamilika Agosti 24.

Habari zinazohusiana