IQNA

Jinai za Isarel

OIC yalaani uvamizi wa Israel dhidi Msikiti wa Al-Aqsa, Yaitaka UN 'ichukue hatua haraka'

21:04 - January 10, 2023
Habari ID: 3476381
TEHRAN (IQNA)-Mkutano wa Wazi wa Kamati ya Utendaji ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Jumanne ulifanyika kuchunguza kuendelea hujuma za Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem), kwa ombi la Dola ya Palestina na Ufalme wa Jordan.

Mkutano huo ulifanyika kwa uratibu na Ufalme wa Saudi Arabia, Mwenyekiti wa Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na Kamati ya Utendaji, katika makao makuu ya OIC, huko Jeddah.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, OIC imelaani "kwa maneno makali kuvamiwa kwa Msikiti uliobarikiwa wa Al  Aqsa na waziri katika baraza la mawaziri la utawala vamizi na wa kikoloni wa Israel, ambaye anajulikana kwa itikadi kali".

OIC ilionya dhidi ya matokeo ya uvamizi unaoendelea, "ikiwa ni pamoja na uchochezi, unyanyasaji unaoendelea, na mashambulizi makubwa ya kila siku ya mamlaka ya kikoloni ya Israel".

OIC pia imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa nafasi yake kama mdhamini wa amani na usalama wa kimataifa, kutekeleza majukumu yake na kuchukua hatua za dharura, bila kuchagua au undumakuwili, kuzuia na kukomesha uchokoezi hatari wa Israel”.

Katika taarifa hiyo, OIC pia imesisitiza kwamba Al-Haram Al-Sharif "ni sehemu ya kipekee ya ibada kwa Waislamu, inayolindwa na sheria za kimataifa na hadhi ya kihistoria na kisheria." Aidha taarifa hiyo imesisitiza kuhusu  "jukumu kuu la Kamati ya Al-Quds chini ya uongozi wa Mfalme wake Mohamed VI, wa Morocco, katika kupinga hatua kali zilizochukuliwa na mamlaka ya uvamizi wa Israel”.

OIC pia ilishutumu "mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya maeneo matakatifu ya Kikristo na mali zao" katika mji unaokaliwa wa Quds.

tamar Ben-Gvir, Waziri mpya wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, Jumanne iliyopita, na ikiwa ni katika wiki yake ya kwanza ya kazi akiwa na kundi jingine la Wazayuni waliokuwa wanasindikizwa na jeshi la utawala huo ghasibu, walifanya uchochezi mkubwa na kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa kwa kuingia msikitini humo bila kujali lolote.

Msikiti wa Al-Aqsa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho muhimu wa Kiislamu na Palestina mjini Beitul Muqaddas na utawala wa Israel unajaribu kuharibu umuhimu huo, lakini kusimama na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala wa Kizayuni na kuufanya ushindwe kufikia malengo yake maovu dhidi ya Waarabu na Waislamu.

3482006

captcha