IQNA

Jinai za Israel

Maandamano yaendelea dhidi ya waziri mkuu katili wa utawala haramu wa Israel

20:46 - January 08, 2023
Habari ID: 3476375
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya Wazayuni wameandamana kupinga baraza jipya la mawaziri la Waziri Mkuu wa Israel lenye misimamo mikali. Baraza hilo jipya la Benjamin Netanyahu linatabiriwa kuanzisha sera hatari katika za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina la 'Israel'.

Washiriki katika maandamano hayo walikuwa wamebeba bango kubwa lenye maandishi yanayosomeka, "Waziri Fisadi", wakiamuashiria Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni Benjamin Netanyahu ambaye alipatikana na hatia ya kupokea hongo, kuhusika na ufisadi, ulaghai na kutokuwa mwaminifu wakati akiwa mamlakani mwaka 2019. 

Waandamanaji wengine aidha walikuwa wakipiga nara na shaari kama: "pamoja tunapinga ufashisti na vitendo vya ubaguzi." Benjamin Netanyahu mwezi uliopita alitangaza baraza lake la mawaziri linalomjumuisha Otzma Yehudit na Noam Wazayuni wenye misimamo mikali. Hii ni katika hali ambayo, ili kuungwa mkono na kuweza kuaminiwa ili kushirikia na vyama vya siasa vyenye misimamo mikali katika utawala wa Kizayuni, Netanyahu ameahidi kuendeleza ajenda zao wanazozitaka. 

Wakati huo huo Benjamin Netanyahu aliye na umri wa miaka 73 amewasilisha taarifa ya sera za serikali yake ambapo ametoa wito wa kupanuliwa ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizoghusubiwa akisema kuwa hiyo ndiyo ajenda kuu ya serikali yake. 

3481996

captcha