IQNA

Jinai za Israel

Indhari kuhusu Israel kuuugeuza Msikiti wa Al-Aqsa kuwa eneo la kijeshi

20:50 - December 29, 2022
Habari ID: 3476325
TEHRAN (IQNA) - Baraza la Wakfu la Jordan katika mji wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel limeonya kwamba utawala wa kibaguzi unaugeuza Msikiti wa Al-Aqsa kuwa eneo la kijeshi.

Katika taarifa yake, baraza hilo lilisema kuwa linafuatilia "ukiukaji hatari unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Al Quds," likibainisha kuwa "mashuhuri zaidi ni uvamizi wa wanasiasa wa Israel ambao wanafuata itikadi kali kuhusiana na Msikiti wa Al-Aqsa."

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanasiasa wa Israel wanaouvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa hutumia sikukuu za Kiyahudi kama kisingizio cha kufichua sera zao za  Uyahudishaji maeneo hayo matakatifu..

"Makundi ya Wayahudi yenye msimamo mkali yalitekeleza ibada za kizushi na za uchochezi, ikiwa ni pamoja na kuimba ndani ya yadi takatifu za Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa," ilisema taarifa hiyo.

Hii ilikuja kufuatia uvamizi wa mamia ya Waisraeli wa mrengo wa kulia wakati wa likizo ya Kiyahudi ya Hanukkah.

Baraza hilo limekuwa likifuatilia "kwa wasiwasi mkubwa" mienendo ya mamlaka ya uvamizi ya Israel na "kampeni za kimfumo za uchochezi" ambazo zinalenga Waislamu kote ulimwenguni.

Baraza la Wakfu la Jordan limetaka Israel kuacha tabia  za "kibaguzi na uchochezi" na kuacha kuwatumia walowezi wenye itikadi kali kutekeleza mipango yao ya Uyahudi kabla ya vita vya kidini kuzuka.

3481861

captcha