IQNA

Matukio ya Afghansitan

Ahmad Masoud asema mji wa Panjshir haujatekwa na Taliban

17:43 - September 04, 2021
Habari ID: 3474256
TEHRAN (IQNA)- Ahmad Masoud, Kiongozi wa Waafghanistan wanaolipinga kundi la Taliban ametoa mwito wa kuendelezwa mapambano dhidi ya kundi hilo.

Ahmad Masoud, ambaye ni mwana wa Ahmad Shah Masoud, shujaa wa taifa wa Afghanistan amesema leo kwamba: "Hatutaacha katu kupambana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, uhuru na uadilifu."

Mkoa wa Panjshir, ndilo eneo pekee ambalo bado halijadhibitiwa na Taliban; na Ahmad Masoud pamoja na Amrullah Saleh, makamu wa rais wa Afghanistan Ashraf Ghani aliyeitoroka nchi, pamoja na wapiganaji wao, wamezatiti ngome zao katika mkoa huo.

Vita na mapigano mkoani Panjshir baina ya wapiganaji wa Taliban na wapinzani wanaoongozwa na Ahmad Masoud yangali yanaendelea huku kila upande ukidai kusonga mbele.

Hayo yanajiri huku Fahim Dashti, msemaji wa vikosi vya wapiganaji wanaolipinga kundi la Taliban akitangaza jana Ijumaa kuwa wapiganaji 450 wa kundi hilo wameuawa na wengine 130 wamekamatwa mateka.

Kwa mujibu wa Dashti wapiganaji wa Taliban wamelazimika kurudi nyuma kutoka mkoa wa Panjshir.

Katika upande mwingine, msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ametangaza kuwa, karibu asilimia 20 ya eneo la mkoa wa Panjshir inadhibitiwa na wapiganaji wa kundi hilo na kwamba wapiganaji wao wanasonga mbele kuelekea makao makuu ya mkoa huo.

Tarehe 15 Agosti, vikosi vya kundi la Taliban viliingia mji mkuu wa Afghanistan Kabul; na sambamba na kuingia vikosi hivyo, rais Ashraf Ghani aliitoroka nchi na hivi sasa amepatiwa hifadhi katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).Ahmad Masoud asema mji wa Panjshir haujatekwa na Taliban

Umoja wa Ulaya na Taliban

Mkuu wa Sera za Kigeni za Umoja wa Ulaya amedai kuwa EU haitalitambua rasmi kundi la Taliban, na badala yake amelipa kundi hilo masharti matano ya kuweza kuwa na mawasiliano nalo, eti kwa maslahi ya wananchi wa Afghanistan.

Josep Borrell alitaja masharti hayo yatakayoiwezesha EU kuwa na eti 'mawasiliano ya kioperesheni' na Taliban jana Ijumaa katika kikao na waandishi wa habari mjini Brdo, Slovenia baada ya kufanyika mkutano usio rasmi wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Amebainisha kuwa: Mustakabali wa Afghanistan linasalia kuwa suala nyeti kwetu. (Mustakabali huo) unatuathiri sisi, eneo na uthabiti wa dunia, kama ambavyo una mfungamano wa moja kwa moja na usalama wa Ulaya. 

Baadhi ya masharti hayo ya EU kwa Taliban yanasema; Mosi, EU inataka hakikisho la serikali ya Afghanistan kwamba nchi hiyo hatageuka kuwa kitovu cha 'ugaidi wa kimataifa; na pia itafuatilia kuona iwapo utawala mpya nchini humo unaheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu hususan haki za wanawake.

Aidha EU inaitaka Taliban iunde serikali jumuishi, mbali na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingizwa nchini humo; na vile vile kuheshimu ahadi yake ya kuruhusu raia wa kigeni na Waafghani walio katika hatari wanaondoka nchini humo.

Marekani na waitifaki wake wamelazimika kukimbia Afghanistan baada ya uvamizi wao wa miaka 20 kutozaa matunda yoyote isipokuwa kupata nguvu ugaidi, vita, ukatili, machafuko, ukosefu wa amani na utulivu pamoja na mauaji ya mamia ya maelfu ya wananchi wa Afghanistan.

3994836

captcha