IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Kijana Muirani katika Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani nchini Bangladesh

19:43 - January 22, 2024
Habari ID: 3478236
IQNA - Seyed Abolfazl Aqdadsi, kijana mhifadhi Qur'ani Tukufu kutoka Iran, anaiwakilisha nchi yake katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Bangladesh.

Aqdasi alipanda jukwaani katika mashindano hayo ili kuonyesha vipaji vyake vya Qur'ani Jumapili jioni.
Aliulizwa maswali tofauti kisha akatakiwa asome aya kadhaa na kuitaja Sura ambamo zimo aya hizo.
Wahifadhi kumi wa Qur'ani kutoka Iran, Bangladesh, Yemen, Syria, Oman, Misri, Algeria, Tanzania, Libya na Jordan wanachuana katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani.
Kundi la wataalamu wa Qur'ani wanaotambulika kimataifa wanatathmini maonyesho ya wapinzani katika maeneo ya kuhifadhi, Sawt, Lahn, Waqf na Ibtida na Tajweed.
Mashindano hayo yanatazamiwa kutangaza kwa mamilioni ya Waislamu nchini Bangladesh wakati wa mwezi ujao wa Ramadhani.
Aqdasi, 15, ni hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka mji wa kaskazini mwa Iran wa Rasht.
Alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka sita na aliweza kuhifadhi Kitabu kitakatifu chote katika miaka miwili.
Mwaka jana, aliiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano ya kimataifa ya mtandaoni ya Qur'ani nchini Algeria.

 
 

 

3486902

Habari zinazohusiana
captcha