IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran kurejea katika ukumbi mkuu wa Tehran

22:29 - October 26, 2022
Habari ID: 3475991
TEHRAN (IQNA) - Ukumbi wa Kimataifa wa Tehran utakuwa mwenyeji wa toleo lijalo la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.

Wakati ukumbi wa mikutano ulitumika kuandaa shindano hilo kwa miaka mingi, ukumbi wa hafla ulibadilika katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu tofauti.

Sasa, kwa mujibu wa Hamid Majidimehr, Mkuu wa Masuala ya Qur'ani katika Shirika la Masuala la Wakfu na Misaada la Iran, mashindano hayo yatarejea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Tehran ambao pia ni maarufu kama  'Ukumbi wa Viongozi.'

Alisema uwezo mkubwa wa ukumbi huo, miundombinu yake mizuri na ufundi, wasimamizi wake wazoefu ni miongoni mwa sababu zilizofanya kuchaguliwa tena kuandaa hafla hiyo adhimu.

Ukumbi huu ulikuwa umejengwa kwa ajili ya kuwakaribisha viongozi wageni wa kigeni hapo awali na hivyo ni mzuri kwa ajili ya kuandaa matukio ya kimataifa kama vile mashindano ya Qur'ani, aliongeza.

Kufanyika mashindano hayo katika ukumbi huo mkuu wa Tehran kutakuwa ni uthibitisho kwamba katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina suhula bora zaidi kwa ajili ya Qur'ani Tukufu, Majidimehr aliendelea kusema.

Fainali Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran imepangwa kuandaliwa ana kwa ana kwa mnasaba wa Mab'ath, katikati ya Februari 2023, afisa huyo alisema hapo awali. Mab'ath ni kumbukumbu ya siku ambayo Mtume Muhammad (SAW) alichaguliwa kuwa mjumbe wa Mungu.

Majidimehr ameyataja mashindano ya Iran kuwa ni mashindano makubwa na yenye sifa kubwa zaidi ya kimataifa ya Qur'ani duniani kwa kuzingatia sio tu idadi ya washindani bali pia asasi yake na vipengele vyake vya kiufundi.

Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada ya Iran hufanya mashindano hayo kila mwaka kwa kushirikisha wahifadhi na wahifadhi Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

3481004

captcha