IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Waislamu wengi wa Marekani wanaunga mkono Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Hamas dhidi ya Israel

13:47 - November 15, 2023
Habari ID: 3477896
Israel WASHINGTON, DC (IQNA) - Asilimia 60 ya Waislamu nchini Marekani wanaunga mkono Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, dhidi ya utawala wa Israel, wakisema kundi hilo la kupigania ukombozi lilikuwa na haki katika mashambulizi yake.

Haya ni kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la Marekani Cygnal.

Hisia hii, iliyopatikana katika uchunguzi huo, inawiana na dhana ya Umma wa Kiislamu, ikisisitiza kuhusu uungaji mkono wa kimataifa kwa Wapalestina.

Utafiti huo ulifanywa baada ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyofanywa na Hamas tarehe 7 Oktoba ikiwa ni jibu kwa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina katika kipindi cha zaidi ya miongo saba.

Baada yah apo utawala katili wa Israel ulianzisha vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Gaza ambapo hadi sasa Wapalestina zaidi ya 11,500, wengi wakiwa ni wanawake na Watoto wameuawa.

Maandamano ya wafuasi wa Palestina yanafanyika karibu kila katika miji kadhaa nchini Marekani kulaani jinai hizo za Israel.

Mapema mwezi Oktoba, uchunguzi wa Cygnal ulifichua mitazamo miongoni mwa Wamarekani Waislamu kuhusu mzozo wa Israel-Palestina. Kulingana na utafiti huu, asilimia 60% ya Wamarekani Waislamu wanaamini kwamba Hamas ilikuwa na haki ya kushambulia ardhi za Palestina zilizopachikwa jina la Israel.

Hasa, mbunge Rashida Tlaib mwenye asili ya Palestina anaunga mkono hisia hii, akisisitiza kwamba vitendo vya Hamas ni mapambano halali  dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Israel.

Utafiti huo unaonyesha upendeleo mkubwa miongoni mwa Wamarekani Waislamu kwa viongozi wa Kiislamu, akiwemo kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh, ikilinganishwa na Rais wa Marekani Joe Biden.

3486029

Habari zinazohusiana
captcha