IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Morocco kuandaa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu

17:19 - August 16, 2023
Habari ID: 3477444
RABAT (IQNA) - Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco imetangaza tarehe ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini humo.

Hafla hiyo ya kimataifa, inayojulikana kama Tuzo ya Kimataifa ya Mohammad VI, itaanza Septemba 12, wizara hiyo ilisema, kulingana na tovuti ya Ahdath Info.
Sherehe ya uzinduzi itafanyika katika Msikiti wa Hassan II huko Casablanca, ilibainisha.
Washindani watashindana katika kategoria za kuhifadhi Qur'anI, kisomo, Tarteel na Tafsir. Wahifadhi na wasomaji wa Qur'ani kutoka Morocco pamoja na nchi nyingine za Afrika, ulimwengu wa Kiarabu, Asia na Ulaya watashiriki katika mashindano hayo, wizara hiyo iliendelea kusema.
Itakuwa ni toleo la 17 la tukio la kimataifa la Qur'ani, ambalo hufanyika kila mwaka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kama sehemu ya juhudi za wizara hiyo kuendeleza kuhifadhi Qur'ani, Tajweed na Tafsir.
Morocco ni nchi ya Kiarabu ya Kaskazini mwa Afrika inayopakana na Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Mediterania.  Uislamu ndiyo dini kuu nchini Morocco, huku asilimia 99 hivi ya watu wakiufuata.
 
4162872

Habari zinazohusiana
Kishikizo: morocco
captcha