IQNA

Wamorocco waandamana kuwaunga mkono Wapalestina, kupinga Israel

6:58 - October 27, 2015
Habari ID: 3395088
Makumi ya maelfu ya raia wa Morocco wamefanya maandamano makubwa mjini Casablanca kupinga hujuma za utawala haramu wa Israel katika msikiti wa al-Aqsa.

. Maandamano hayo yaliandaliwa na Muungano wa Waislamu na yaliwashirikisha wanasiasa na wasomi wa taaluma mbalimbali. Waandamanaji wametoa nara za kulaani utawala wa Kizayuni wa Israel sambamba na kuchoma moto bendera ya utawala huo pamoja na Marekani.
Waandamanaji pia wametangaza uungaji mkono wao kwa Wapalestina na kutoa wito kwa nchi za Kiislamu kuuhami msikiti mtakatifu wa al-Aqsa. Baadhi ya mabango ya waandamanaji yamemlaani Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na kumtaja kuwa muuaji nambari moja.
Tangu kuanza hujuma mpya ya Wazayuni katika msikiti wa al-Aqsa mwanzoni mwa mwezi huu, tayari Wapalestina wasiopungua 60 wameuawa shahidi na wengine wengi wamejeruhiwa huku jamii ya kimataifa ikiendelea kubakia kimya.

3395005

captcha