IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran

Mafanikio ya Iran yamepelekea adui azidishe mashinikizo ya pande zote

17:00 - May 19, 2023
Habari ID: 3477018
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran aliyataja mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ndio sababu kuu ya vita mseto na mashinikizo ya pande zote ya maadui.

Hujjatul-Islam Kazem Seddiqi ameongeza kuwa: "Adui amekuja uwanjani akiwa na zana zote zinazowezekana ili kuwakatisha tamaa watu wa Iran na kuanzisha vita vya kisaikolojia, lakini pamoja na hayo, taifa shujaa la Iran bado liko uwanjani na linasimama kidete kupimbana na adui."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema, ili kufikia malengo ya Mwenyezi Mungu ni lazima kuyashinda na kuyavuka magumu na mashaka ya aina mbalimbali, na kuongeza kuwa: “Mafanikio hupatikana kwa kusimama imara na kupambana, na hakuna taifa lililopata mafanikio bila ya kuwa na subira na kudumisha mapambano."

Hujjatul Islam Seddiqi ameeleza kuwa, wale wanaopotosha ukweli wa dini na Mapinduzi ya Kiislamu na kuwafanya waja wa Mwenyezi Mungu watupilie mbali utambulisho wao ni watu wa giza, na akasema: "Vita mseto vya maadui dhidi ya Iran ya Kiislamu ni ushahidi kwamba tunakaribia kileleni."

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran pia amewapongeza Waislamu hususan wafuasi na wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume wetu Muhammad (saw) kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mjukuu wake, Bibi Fatima Masouma, akimtaja kuwa alikuwa shakhsia wa aina yake.

Amegusia sababu ya siku ya kuzaliwa mjukuu huyo wa Mtume (saw) kupewa jina la "Siku ya Taifa ya Wasichana" na akasema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewapa wasichana umuhimu mkubwa na makhsusi.  

Amesema: Wasichana na mabinti ni mama wa mashahidi wanaouliwa katika njia ya Allah, walezi wa wasomi, mashujaa na mawalii wa Mwenyezi Mungu; kwa sababu msingi wa saada na ufanisi upo katika malezi ya akina mama.

captcha