IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Kufeli Marekani katika kuunda muungano dhidi ya Iran ya Kiislamu ni nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu

22:59 - May 05, 2023
Habari ID: 3476960
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ametaja kufeli Marekani katika kuziunganisha nchi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni ushindi au nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akaongeza kuwa: "Kumfuata Wali ul Amr wa Waislamu na Hujja za Kisharia ni mfano wa usaidizi wa Mwenyezi Mungu."

Akigusia safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Syria, Ayatullah Seyed Ahmad Khatami, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran  ameongeza kuwa: Ziara hii ni uthibitisho mwingine wa misimamo imara ya mrengo wa muqawama au mapambano; hasa kwa vile Syria iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni."
Ayatullah Khatami amesema: "Hatua ya wananchi wa Syria kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  kwa namna ya kipekee kwa hakika ni kulienzi na kulitukuza taifa la Iran na kunaonyesha mafungamano makubwa kati ya mataifa haya mawili na shukrani za Wasyria kwa uungaji mkono wa taifa la Iran wakati nchi hiyo ilipokuwa ikikabiliana na dhulma."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: "Kuzidi kuimarika uhusiano kati ya Iran na Syria katika nyanja zote kumedhihirisha kuzaa matunda nasaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu za kuendelea kuupinga utawala ghasibu wa Kizayuni, kwani madola yote yalikuwa dhidi ya Syria na nchi pekee  iliyosimama karibu na Syria, ilikuwa ni Iran ya Kiislamu."

4138649

captcha