IQNA

Kususia bidhaa za Israel

Waislamu watakiwa kususia tende za Israel mwezi wa Ramadhani

18:02 - February 26, 2023
Habari ID: 3476629
TEHRAN (IQNA) – Kampeni mpya ya kususia utawala wa Kizayuni imezinduliwa ili kuwataka Waislamu barani Ulaya na maeneo mengine duniani kuangalia lebo za matunda hasa tende na kuepuka kununua tende za utawala haramu wa Israel katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu wanapaswa kuhakikisha kuwa hawafuturu kwa bidhaa za "ubaguzi wa rangi," waandaaji wa kampeni hiyo wamesema.

"Kwa kuchagua kutonunua tende za Israel katika mwezi huu wa Ramadhani, Waislamu wanaweza kutuma ujumbe wa wazi na wenye nguvu wa kulaani vitendo vya Israel uvamizi na ukaliaji haramu, l na ubaguzi wa rangi huko Palestina," alisema Shamiul Joarder wa Jumuiya ya Marafiki wa Al-Aqsa (FOA) yenye makao yake nchini Uingereza.

Taarifa hiyo imebaini kuwa "Israel ndio mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa tende aina ya Medjool, na asilimia 50 ya tende za Israeli zinauzwa Ulaya. "Tende hizi zinauzwa katika maduka makubwa makubwa pamoja na maduka madogo katika bara zima la Ulaya."

FOA iliongeza kuwa asilimia 50 ya tende za Israel zinasafirishwa kwenda Ulaya, ambapo Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Uhispania na Italia huagiza kiasi kikubwa cha tende hizo zilizokaushwa. Mnamo 2020 Uingereza iliagiza zaidi ya tani 3,000 za tende kutoka Israeli, zenye thamani ya takriban pauni milioni 7.5.

Taarifa hiyo pia ilibainisha kuwa hadi sasa mwaka huu, Israel imewaua shahidi Wapalestina wasiopungua 62 wakiwemo watoto 13 - sawa na mtoto mmoja kila baada ya siku tano.

"Utawala wa Israel inaongeza ubomoaji wa nyumba kwa kasi ya kutisha na imeahidi kupanua makazi haramu kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa," iliongeza.

FOA ilisisitiza kwamba mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Amnesty International na Human Rights Watch, "yamesema kuwa Israel inatenda uhalifu wa ubaguzi wa rangi, lakini mataifa ya Ulaya yanashindwa kuiwekea Israel vikwazo."

Joarder alisema: "Ni wakati wa kutangaza upya ahadi yetu ya kuunga mkono Harakati ya Kimatiafa ya Kususia Israel (BDS)  Ramadhani hii. Lazima tukumbuke kuwa kama jumuiya tuna nguvu - tunaweza kufanya sauti zetu zisikike kupitia kitendo rahisi cha kutotumia tende za Israel."

Aliongeza: "Tunachohitaji kufanya ni #CheckTheLabel na sio kununua tende kutoka utawala wa Israel ambao ni utawala wa ubaguzi wa rangi."

Siku ya kuwahimiza Waislamu "kuangalia lebo" (#CheckTheLabel ) imeandaliwa kwenye misikiti ya Uingereza mnamo Machi 17, Ijumaa ya mwisho kabla ya Ramadhani. Pia kutakuwa na harakati ya mtandaoni ya uhamasishaji wikendi ya mwisho kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kishikizo: tende BDS israel
captcha