IQNA

Waislamu Pakistan

Serikali ya Pakistani kufuatilia tarjuma za Qur'ani Tukufu Tukufu kwenye mitandao kijamii

11:11 - January 06, 2023
Habari ID: 3476362
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Pakistan itafuatilia tarjuma za Qur'ani Tukufu zilizo katika mitandao ya kijamii nchini humo ili kuhakikisha kuwa ni shahihi kwenye mitandao ya kijamii.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Rana Sanaullah na Waziri wa Shirikisho wa Masuala ya Kidini Mufti Abdul Shakoor walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Islamabad siku ya Alhamisi.

Sanaullah alisema kuwa Wizara ya Masuala ya Kidini imetayarisha toleo sahihi la Qur'ani Tukufu, ambalo linatazamiwa kuidhinishwa na Bodi ya Qur'ani. Hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya watu wamekuwa wakiweka katika mitandao ya kijamii tarjuma na tafsiri ya Qur'ani Tukufu kulingana na matakwa yao.

Mamlaka ya Mawasiliano ya Pakistani (PTA) itashirikiana na Wizara ya Masuala ya Kidini kuhakikkisha kuwa agizo hilo linatekelezwa.

Sanaullah alisema tarjuma sahihi ya Qur'ani Tukufu itawasilishwa kwa kila wilaya na huku akiongoza kuwa ni wajibu wa serikali kufanikisha jambo hilo.

Akizungumzia jukumu la mahakama ya Lahore, Shakoor alisema, "LHC imefanya kazi kubwa katika suala hili. Tayari tuko makini katika kulinda Kurani Tukufu kwani ni wajibu wetu wa kidini."

348196

captcha