IQNA

Siku Kuu ya Krismasi

Maonyesho ya Kaligrafia Mtandaoni Yanaashiria Kuzaliwa Nabi Isa (Yesu)

19:23 - December 25, 2022
Habari ID: 3476305
TEHRAN (IQNA) – Katika mnasaba wa siku ya kuzaliwa Nabii Isa ibn Maryam –Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake-AS-, maonyesho ya kaligrafia yenye maandishi ya maandishi kuhusu Bibi Maryam (SA) yamezinduliwa na Shirika la Qur'ani la Wanaakademia wa Iran.

Maoneysho hayo yanayoashiria  siku ya kuzaliwa kwa Nabi Isa mwana wa Maryam (AS) na mwanzo wa mwaka mpya wa Miladia, yanalenga kuhimiza amani na kuishi pamoja kwa amani.

Kazi ishirini na moja za kaligrafia za wasanii 20 wa Iran zinaonyeshwa kwenye maonyesho ya mtandaoni.

Wanakaligrafia hao ni pamoja na Aria Soltani, Amin Zanjani, Nima Hassanpour, Amir Danesh Maraqi, Ali Reza Karimian, Farshad Heidari, Robabeh Zeinali, Mahmoud Jalali, Roqayyeh Sadat Vaziri, Sattar Valinejad, Hamed Shah Hosseini, Hossein Alimarrimidan, Mehsen Kahrrimidad, Mehsen Kahrrimidad Ali Mardani, Gholam Reza Sadeqi, Arian Mahzoun, Hamid Andalib, Seyed Mohsen Rouhani na Mehdi Ezzati.

Kazi zinazoonyeshwa ziko katika mitindo ya maandishi ya Nastaliq, Nastaliq iliyovunjika, Naskh na Thulth ambayo ni maandishi ya Kiislamu na Iran.

Ili kutembelea maonyesho ya mtandaoni, ingia kwenye maonyesho bonyeza anuani hii http://exhibition.isqa.ir/index.php?newsid=44

Jina la Maryam (SA) limetajwa katika Sura kadhaa za Qur'ani Tukufu, zikiwemo Sura An-Nisa, At-Tawbah, Al Imran na Al-Ma’idah.

Katika Aya ya 34 ya Surah Maryam (19), Mwenyezi Mungu anasema: “Huyo alikuwa (Nabii) Isa bin Maryamu. Kauli ya kweli katika yale wanayoyatilia shaka".

Online Calligraphy Expo Marks Birthday of Jesus  

Wakristo kote duniani hii leo wanaadhimisha sikukuu yao ya Krisimasi wanayoinasibisha na siku ya kuzaliwa Nabii Isa Masih AS, sherehe ambazo hufanyika tarehe 25 Disemba kila mwaka.

Wakatoliki na Waprotestanti huadhimisha Krismasi Disemba 25, huku Waothodoksi wakiadhimisha kumbukumbu ya mazazi hayo ya  Isa Masih (AS) Januari 7.

Isa Masih (AS) ni mmoja wa Mitume wakubwa wa Mwenyezi Mungu ambaye ametajwa kwa heshima na taadhima kubwa katika Qur'ani Tukufu, na inamtambulisha kama mmoja wa Manabii wakuu waliopewa Kitabu na sheria na Mwenyezi Mungu.

captcha