IQNA

Wito wa kusisia tende za utawala haramu wa Israel

18:12 - March 20, 2022
Habari ID: 3475059
TEHRAN (IQNA)- Wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani unapokaribia, mkuu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu (IHRC) yenye makao yake mjini London amehimiza kususia tende zinazozalishwa na makampuni ya utawala haramu wa Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.

Katika ujumbe, mkuu wa tume hiyo, Masoud Shajareh anabainisha kuwa ni muhimu kuongeza ufahamu kuhusu kutonunua tende kama hizo.

Wakati huo huo, IHRC imeyaandikia barua maduka makubwa ya Uingereza kuyakumbusha juu ya wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa kuhakikisha hayauzi tende zinazozalishwa na makampuni ya Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhani unapokaribia ambapo Waislamu kwa kahutumia kwa wingi tende hasa wakati wa kufuturu, maduka makubwa na maduka kila mahali yataona ongezeko la mauzo ya matunda hayo.

Inakadiriwa kuwa 60% ya tende za Israel hutoka katika mashamba ya walowezi wa Kizayuni ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala huo wa Kizayuni.

Vitongoji hivyo vimejengwa kwenye ardhi iliyoibwa kutoka kwa Wapalestina, ambao nyumba zao na mali nyingine mara nyingi hubomolewa ili kupisha nyumba na biashara zinazomilikiwa na walowezi haramu wa Kizayuni. Ni ardhi ambayo jumuiya ya kimataifa na sheria za kimataifa zinaichukulia kama mali ya Wapalestina, na chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Palestina.

Mara nyingi makampuni hayo yanahusika katika ukiukaji wa haki za wafanyakazi pia, yakiwanyonya Wapalestina maskini kutoka Ukingo wa Magharibi. Katika visa vingi wafanyakazi hujumuisha watoto walio na umri wa miaka 11, ambao wanapendelewa kuliko watu wazima kwa kuwa ni rahisi kuwadhalilisha na mara nyingi wako tayari kufanya kazi chini ya mazingira magumu..

Barua hiyo pia inasema ni muhimu kwa watumiaji kujua asili ya bidhaa wanazonunua ili waweze kufanya uamuzi sahihi kwa kuzingatia maadili. Kwa madhumuni haya, IHRC na NGOs nyingine zimekusanya orodha ya wazalishaji wenye hatia pamoja na wale ambao hawakiuki sheria za kimataifa.

Ili kuficha asili ya bidhaa zao, baadhi ya makampuni yameamua kuzipa jina kama "Made in Palestine" au "Produce of Palestine", wakati kwa hakika zinazalishwa katika utawala haramu wa Israel au mara nyingi zaidi hukuzwa ndani ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Kwa sasa ni kinyume cha sheria chini ya sheria ya Uingereza kuuza bidhaa za vyakula vilivyopakiwa bila lebo ifaayo, inayojumuisha jina sahihi la biashara inayohusika na bidhaa hiyo na nchi yake ya asili.

Amnesty International hivi karibuni ilitoa ripoti inayorejea matokeo ambayo tayari yamekubaliwa na NGOs maarufu za kimataifa za haki za binadamu; Human Rights Watch na War On Want, pamoja na NGOs sawa za Israeli; B'Tselem na Yesh Din, kwamba za utawala haramu wa Israel kwa Wapalestina ni sawa na ubaguzi wa rangi.

Barua hiyo inazitaka maduka makubwa kuwajibika na kulichukulia kwa uzito suala la haki za binadamu.

3478243

Kishikizo: israel BDS palestina
captcha