IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanawake nchini Kyrgyzstan

15:26 - December 20, 2021
Habari ID: 3474698
TEHRAN (IQNA) – Duru ya kwanza ya mashindano yay a kitaifa ya wanawake itafanyika nchini Kyrgyzstan.

Mashindano hayo yameandaliwa na Idara ya Masuala ya Kidini Kyrgyzstan kwa ushirikiano na Taasisi ya Darul Qur'an.

Kategoria ya mashindano hayo itakuwa ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu na kuhifadhi juzuu 15.

Mashindano hayo yanaanza Disemba 22 na yataendelea hadi Disemba 26. Washindi watapata zawadi ya fedha taslimu na tiketi ka kutekeleza Hija ndogo ya Umrah.

Mashindano hayo ya Qur'ani yatafanyika katika Msikiti wa Imam Sarakhsi katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek.

Kyrgyzstan ni nchi iliyo katika eneo la Asia ya Kati ambapo asilimia 86 ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu.

4022217

captcha