IQNA

Daktari Muislamu adungwa kisu Manchester, Uingereza

13:37 - September 25, 2017
Habari ID: 3471191
TEHRAN (IQNA)-Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wamemdunga kisu na kumjeruhi daktari Muislamu katika mji wa Manchester nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa, Daktari Nasser Kurdi, mtaalamu bingwa wa masuala ya mifupa alidungwa kisu Jumapili usiku akielekea kuswali nje ya Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu, katika eneo la Hale mjini Manchester.

Alikimbizwa hospitalini punde baada ya tukio hilo na kupata na hali yake inaendelea kuboreka.

Polisi mjini Manchester wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo na tayari watu wawili wameshakamatwa.

Jumuiya ya Waislamu wa Altrincham na Hale (AHMA) imetoa taarifa na kusema kabla ya kuhujuma hiyo mtu alisikika akitoa matamshi yenye chuki. Bw. Akram Malik mwenyekiti wa AHMA amesema: "Inasikitisha kuwa kuna mwanachama wa jamii yetu amedungwa kisu wakati akielekea kuswali."

"Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampe shifaa Daktari Kurdi na waliotekeelza hujuma hiyo washughulikiwe kikamilifu na mkono wa sheria. Nato wito kwa Waislamu wakabiliana na hujuma kama hizo za chuki kwa mapenzi."

Daktari Kurdi ambayo ni naibu mwenyekiti wa AHMA amewahi kutoa hotuba za Ijumaa katika msikiti wa Kituo cha Utamaduni cha Kiislamu eneo la Hale na ni nguzo muhimu ya jamii ya Waislamu. Aidha amekuwa mstari wa mbele kuhimiza Waislamu waishi kwa ujirani mwema na watu wa jamii zingine.

Katika miaka ya karibuni, mbali na Uingereza, chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na mashambulio ya mitaani dhidi ya Waislamu na wahajiri yameongezeka mnokatika nchi zingine za Ulaya.

3646015

captcha