Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yamefadhiliwa na Taasisi ya Al Maalumat ambayo inafungamana na Taasisi ya Kutoa Misaada ya Dar al Ber.
Mashindano hayo yatawashirikisha watu ambao wameikubali dini tukufu ya Kiislamu maishani na ambao wanapata au wamepata mafundisho ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani katika taasisi zinazofungamana na Dar al Ber kote Imarati.
Aidha waliosilimu ambao ni wafanyakazi wa idara za serikali na taasisi mbali mbali Imarati pia wanaweza kujisajili katika mashindano hayo.
Taasisi ya Al Maalumat imesema tarehe ya mwisho ya kujisajili kushiriki katika mashindano hayo ni tarehe 12 Novemba 2016.
Mashindano hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika Imarati maalumu ya waliosilimu
yatakuwa na zawadi za fedha taslimu zaidi ya
AED 50,000
kwa washindi wa kwanza 10 katika kila kategoria.