IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya wasichana kufanyika Dubai

20:04 - August 02, 2016
Habari ID: 3470488
Awamu ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu maalumu kwa wasichana yamepangwa kufanyika Dubai nchini Imarati kuanzia Novemba 6 hadi 18.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yajulikanayo kama Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wasichana ya Sheikha Fatima Bint Mubarak yatasimamiwa na Kamati Andalizi ya Zawadi ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai (DIHQA). Ibrahim Mohammaed Bu Melha, Mshauri wa Mtawala wa Dubai katika masuala ya utamaduni ambaye pia ni mkuu wa kamati andalizi ya DIQHA, siku ya Jumatatu alizundia bango la mashindano hayo.

Dkt. Melha amesema mashindano hayo yanafanyika kama njia ya kutambua jitihada zisizo na kikomo za Sheikh Fatima katika kuhudumia Uislamu na Qur’ani Tukufu.

Aidha amesema mashindano hayo ni fursa kwa wasichana wa Imarati na dunia nzima kushindana katika kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu. Hapo kabla mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Dubai yalikuwa ya wanaume pekee.

Awamu ya kwanza ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu maalumu kwa wasichana itakuwa kwa wale wenye umri wa chini ya miaka 25. Maelezo zaidi kuhusu mashindano hayo yanapatikana katika tovuti ya www.quran.gov.ae.

3460573

captcha