IQNA

Nchi za Kiislamu Zataka Bidhaa za Utawala wa Kizayuni zisusiwe kimataifa

19:19 - March 08, 2016
Habari ID: 3470186
Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC imetoa wito wa kususiwa bidhaa za zinazozalishwa na utawala haramu wa Israel aktika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Katika taarifa, nchi za Kiislamu duniani zimetoa wito kwa jamii ya kimataifa nan chi wanachama kususia na kupiga marufuku bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji walowezi wa Kizayuni.

Taarifa hiyo imetolewa katika Kikao cha tano cha dharura cha wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichomalizika juzi katika mji mkuu wa Indonesia Jakarta.

Maudhui kuu ya mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya wawakilishi 500 wa nchi 57 za Kiislamu ilikuwa ni "Palestina na Quds Tukufu".

Aidha OIC ilitoa wito wa kuwepo himaya kamili ya kisiasa, kidiplomasia, na kisheria ili kuhakikisha Wapalestina wanapata haki zao zisizopingika

Mwezi uliopita mamia ya Wapalestina waliandamana katika Ukingo wa Magharibi wakitaka bidaa za utawala haramu wa Israel zisusiwe.

Ujenzi wa vitongoji vya Wayahudi katika ardhi za Palestina huwa na maana ya kutwaliwa mashamba, nyumba na ardhi za Palestina, kwa msingi huo kila mwaka Wapalestina wengi wamekuwa wakilazimishwa kuhama na kuwa wakimbizi kutokana na siasa hizo za kibaguzi za Israel.

Ni kwa sababu hiyo pia ndiyo maana jumuiya kadhaa za kimataifa zikaanzisha kampenzi iliyopewa jina la 'Susia Israel' ili kulalamikia siasa hizo za kutaka kujitanua za utawala wa kibaguzi wa Israel.

3481621

captcha