IQNA

Israel ni chanzo cha machafuko katika eneo

6:19 - August 14, 2015
Habari ID: 3342896
Katibu Mkuu wa Baraza la Kiislamu na Kikristo la Kutetea Quds Tukufu amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ni chanzo cha machafuko na ghasia katika eneo la Mashariki ya Kati.

Akizungumza na tovuti ya 'Palestine Online' Hanan Issa amesema njama za hivi karibuni za  Israel za kuyahudisha Quds Tukufu ni hatua ya kulitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati katika machafuko.
Msomi huyo wa sheria za kimataifa amesema utawala ghasibu wa Israel unapaswa kuwajibishwa kutokana na hali mbaya katika eneo la Mashariki ya Kati. Amesema utawala wa Israel na walowezi wa Kizayuni wanatumia njia mbali mbali kuwasukuma Wapalestina waingie katika vita na mauaji.
Bi.Hannan Issa amesema hatua ya Waziri wa Vita wa Israel Moshe Yaalon kuhujumu Masjid Ibrahimi katika mji wa Al Khalil na kuutnagaza msikiti huo kuwa eneo la kijeshi ni njia moja ya kujaribu kuhalalisha hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya ibada. Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unapanga kubadilisha Masjid Ibrahimi kuwa  hekali la . Aidha mwanaharakati huyo Mpalestina Mkristo ameonya kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unatekeleza njama za kuharibu Masjid  al Aqsa na mahala mpake kujenga hekali bandia la Kiyahudi.../mh

3341697

captcha