IQNA

Utalii wa Kiislamu

Dubai yatangaza Msikiti wa kwanza wa chini ya maji duniani

22:03 - September 22, 2023
Habari ID: 3477633
DUBAI (IQNA) - Dubai inatazamiwa kuzindia msikiti wa kwanza duniani unaoelea kwa gharama inayokadiriwa ya takriban Dh55 milioni.

Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za Hisani huko Dubai imetangaza mradi kabambe wa Utalii wa Kiislam unaolenga  kuimarisha utalii wa Kiislamu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)..

Msikiti huo, umepangwa kukamilika mnamo 2024 ambapo muundo wake unajumuisha ghorofa tatu, kila moja ikitumikia kwa lengo maalumu. Ghorofa ya kwanza ni eneo la sala , ghorofa ya pili ni ukumbi wa shughuli mbali mbali , na ghorofa ya tatu ina maonyesho ya Kiislamu. Msikito huo wa chini ya maji utakuwa na uwezo wa kuhudumia waumini  kati ya 50 hadi 75 kwa wakati moja na mradi huu wa ajabu unaahidi kuleta mwanga wa utulivu wa kiroho na uboreshaji wa kitamaduni.

Zaidi ya hayo, msikiti huo utakuwa na maonyesho ya Qur'ani yanayoelezea safari ya Msahafu wa Sheikh Maktoum bin Rashid Al Maktoum tangu kuzinduliwa kwake hadi usambazaji wa nakala za  Msahafu huo hivi karibuni duniani kote.

Mradi huo wa kihistoria ulitangazwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi  na kuhudhuriwa na maafisa, akiwemo Dk Hamad Al Sheikh Ahmed Al Shaibani, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za Hisani huko Dubai, na watu wengine mashuhuri kutoka idara mbalimbali.

"Mradi wa Utalii wa Kidini huko Dubai" unalenga kukuza hadhi ya Dubai kama kitovu cha utalii wa kidini, kuwakaribisha wageni wa asili zote.

Dk Abdullah Ibrahim Abdul Jabbar, Mkuu wa Mpango wa Utalii wa Kidini, alisema kuwa mradi huo unajumuisha mfululizo wa mipango, ikiwa ni pamoja na Dubai Iftar, mkusanyiko wa kipekee wa wawakilishi wa kidini, na kutembelea misikiti ya kihistoria, mipya na mashuhuri. Pia inaangazia programu za kijamii, michezo na elimu ndani ya mpango wa "Halal Ramadhani", kukuza umoja na mabadilishano ya  kitamaduni.

نخستین مسجد زیر آب در جهان در دبی ساخته می‌شود

نخستین مسجد زیر آب در جهان در دبی ساخته می‌شود

نخستین مسجد زیر آب در جهان در دبی ساخته می‌شودنخستین مسجد زیر آب در جهان در دبی ساخته می‌شود

/3485270

Kishikizo: dubai msikiti
captcha