IQNA

Washiriki kutoka nchi 96 katika Mashindano ya Qur'ani ya Dubai

11:25 - May 09, 2017
Habari ID: 3470973
TEHRAN (IQNA)-Wawakilishi kutoka nchi 96 wamethibitisha kushiriki katika Mashindano ya 21 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Tangazo hilo limetolewa na Ibrahim Mohammed Bu Melha, mshauri wa mtawala wa Dubai katika masuala ya Utamaduni na Kibinadamu ambaye ni mkuu wa kamati andalizi ya mashindano hayo ambayo rasmi yanajulikana kama Zawadi ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Dubai (DIHQA).

Mashindano hayo yanatazamiwa kuanza tarehe 1 na kuendelea hadi 20 katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika ukumbi wa Idara ya Biashara na Viwanda ya Dubai. Mashindano hayo yanafanyika kwa hisani ya Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ambaye pia ni mtawala wa Dubai.

Kamati andalizi ya DIHQA imesema nchi 120 zimealikwa katika mashindano kutoka mabara ya Ulaya, Amerika, Afrika na Asia. Washiriki hawapaswi kuwa juu ya umri wa miaka 25 wakati wa mashindano na wanapaswa kuwa wamehifadhi Qur'ani kikamlifu.

Prof Dr Mohammed Abdulrahim Sultan Alolama mwanachama wa kamati andalizi ya DIHQA na mkuu wa kitengo cha mashindano amesema tayari majaji wa mashindano wameshateuliwa.

Imedokezwa kuwa watakaoshika nafasi za 1-3 watapata zawadi za fedha taslimu Dh250,000, Dh200,000 na Dh150,000 kwa taratibu. Aidha kila mshiriki pia atapata zawadi za fedha taslimu kwa kutegemea pointi watakazopata.

3462778

captcha